UZINDUZI HUU MKUBWA REKODI YAVUNJWA KWA MARA NYINGINE TENA

 Na Mwandishi Wetu 

Leo Tarehe 4 Juni 2021,  Mtandao namba moja wa Kidigitali Tigo kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Infinix wamezindua Simu mpya ya Infinix Note 10 na Infinix Note 10 Pro katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Es Salaam. Akizungumza katika Uzinduzi wa Simu hizo Meneja wa bidhaa za Intaneti kutoka Tigo Bwana Mkumbo Myonga amesema tigo kama kampuni inayotoa Huduma za mawasiliano  uhakikisha wanawaletea Wateja wao simu zenye ubora mkubwa na kuondoa shida ambazo wateja ukumbana nazo katika utumiaji wa huduma za Kidigitali pamoja na kuchochea matumizi ya Kidigitali 

"Mteja akinunua simu hizi katika maduka yetu ya Tigo atajipatia ofa ya Intaneti bure mwaka mzima,  tutampatia mteja Wetu GB 78 BURE mwaka ambapo atapewa takribani GB 6 na nusu za kutumia kila mwezi, simu hizi zinapatikana kwa bei nafuu sana lakini Tigo tunampa mteja Ofa zaidi kwa kumfanyia Service Bure pale simu yake itakapopata tatizo ndani ya miezi 12" alisema Bwana Mkumbo. 

Simu za Infinix NOTE 10 na Infinix Note 10 PRO zitapatikana katika maduka ya TIGO na Infinix kuanzia Jumatatu ya Tarehe 7, June 2021. 


Kwa upande Mwingine Afisa  Mahusiano kutoka kampuni ya Infinix Bi. Aisha Karupa amewapongeza kampuni ya Tigo Kwa utayari wao wa kuzipa kipaumbele bidhaa za Infinix na kuelezea sifa kedekede za Simu hii mpya ya Infinix Note 10 na Infinix NOTE 10 PRO 

" Simu ya Infinix NOTE 10 na NOTE 10 PRO umetengenezwa kwa teknolojia ya Hali ya juu ambapo ina processor kubwa ya G95 kuliko simu zote tulizowahi kutoa hapo awali, Camera ya 64 Mega Pixels hii husaidia kupiga picha nzuri na za kuvutia,  RAM GB 8, na Memory GB 128 pamoja na sifa nyingine nyingi"

Alisema Bi Aisha Karupa

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post