TIGO WALIVYOMWAGA MAMILIONI KWA WASHINDI HAWA 10 , PROMOSHENI YA SHEHEREKEA PESA NA TIGO PESA

 Na Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Jumla ya washindi 10 wa Promosheni ya Sherekea Pesa na Tigo Pesa wamejishindia kiasi cha Shilingi milioni 100 katika droo kubwa inayoendeshwa  kampuni ya Mawasiliao Tigo.Promosheni hiyo iliyodumu kwa wiki 10, ilihusisha washindi zaidi ya 90 wa kila wiki ambao wameshindanishwa katika droo kubwa na kushuhudia washindi kumi wakiondoka na milioni 10 kila mmoja.

Akiziungumza wakati wa hafla ya kutangaza washindi hao,Meneja wa wateja maalumu wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema promosheni ya Sherehekea Pesa ni sehemu ya sherehe ya miaka 10 ya Tigo Pesa nchini Tanzania ambapo ililenga kuwashukuru wateja wake kwa kutumia huduma hiyo.

“Tumekuwa tukiendesha droo za kila wiki kwa wiki 10 mfululizo na hii ni droo kubwa ambayo iliwashindanisha washindi wa wiki kutoka katika mikoa mbalimbali nchi nzima na washindi wa leo watajipatia milioni 10 kila mmoja,” alisema.


“Mteja wa Tigo anavyotumia Tigo Pesa kwa kulipa malipo ya bili, manunuzi ya bidhaa na huduma, kutuma pesa kwa wateja wengine wa Tigo Pesa, kupokea pesa kutoka benki, mitandao mingine na nchi zingine, ndivyo alivyoweza kupata nafasi zaidi kushinda zawadi za pesa. ”alisema.

Aliongeza kuwa katika promosheni hiyo jumla ya kiasi cha Shilingi 200 milioni zimetolewa kwa washindi wa wiki 10 ambao walijishindia Shilingi milioni 1 kila mmoja katika muda wa wiki 9 na droo kubwa ya wiki ya 10 wakajizolea milion 10 kila mmoja.


Mmoja wa washindi Katumu Nembo ambaye ni mamalishe aliishukuru Tigo kwa kuja na promosheni hiyo na kwamba pesa alizopata zitakuwa msaada mkubwa katika kujiendeleza kiuchumi.


“Nimefurahi sana kushinda kiasi hiki cha pesa na nitatumia pesa hii kuboresha biashara yangu na kumaliza kibanda (nyumba) change,” alisema kwa furaha.


Naye, Mandela Charles mkazi wa Tangi bovu Dar es Salaam alisema atatumia kiasi hich cha pesa kuwekeza zaidi kwenye biashara yake huku George Mwijage wa Tanga akisema kitamsaidia kujiendeleza kimasomo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post