DC MPOGOLO APOKELEWA KWA KISHINDO WILAYANI SAME

  Na Mwandishi Wetu


                                            MATUKIO KATIKA PICHA


Wachungaji wakiomba kwa ajili ya kumkabidhi Mhe. Edward Mpogolo ( Mkuu wa Wilaya ya Same) mikononi mwa Mungu , ili amlinde na kumfanikishia katika majukumu ya kuiongoza wilaya hiyo. Maombi hayo yameambatana na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake.  Ikiwa ni ziara yake ya kwanza wilayani hapo
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Edward Mpogolo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za CCM (Wilaya ya Same) alipokwenda kujitambulisha kwa Viongozi na wanachama.  Ikiwa ni ziara yake ya kwanza wilayani hapo


Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.  Edward Mpogolo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi BAKWATA wilayani hapo alipokwenda kujitambulisha. Ikiwa ni ziara yake ya kwanza wilayani hapo


......................................************************...........................................
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.  Edward Mpogolo Amefanya ziara yake ya kwanza wilayani hapo , zikiwa ni siku chache baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan . Mheshimiwa Mpogolo ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Jimbo la Kaskazini Mashariki mwa Tanzania , Ofisi za BAKWATA , Ofisi za CCM n.k


Katika Hotuba yake akiwa katika Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Jimbo la Kaskazini Mashariki mwa Tanzania zilizopo Mjini Same , Mheshimiwa  Mpogolo ameliomba Kanisa kuendelea kuomba kwa ajili ya Serikali lakini pia juu ya wimbi la Tatu la Janga la Corona, na kusisitiza kuendelea kuchukua tahadhari.Ikumbukwe hayo yote yamefanyika ikiwa ni ziara yake ya Kwanza , siku chache baada ya Kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post