Ubalozi wa Sweden wakutanisha Wanafunzi Kisimiri,Ilboru katika mdahalo kwa njia ya Zoom

Wanafunzi wa shule ya sekondari Ilboru na Kisimiri wakiwa katika mdahalo kwa njia ya Zoom na wanafunzi wenzao wa Sweden, Kama wanavyoonekana kwenye TV


 Na Seif Mangwangi, Arusha

Ubalozi wa Sweden kupitia programu yake ya elimu umewezesha wanafunzi wa shule za sekondari za Kisimiri na Ilboru kufanya mdahalo kwa njia ya mtandao wa Zoom na wanafunzi wenzao nchini Sweden kutoka shule ya sekondari ya Skapaskolan iliyopo katoka mji wa Huddinge.

Mdahalo huo ulikuwa na lengo la kubadilishana mawazo na ujuzi wa kimasomo umefanyika leo Mei10, 2021 katika chumba maalum Cha mikutano kilichopo katika hospitali ya Mkoa Mount Meru.

Katika mdahalo huo wa saa2, ulioanza saa4 Hadi saa6 mchana, wanafunzi wote wameeleza mifumo ya elimu katika shule zao na namna ambavyo wazazi wamekuwa wakitoa michango yao katika masomo.

Akizungumza baada ya mdahalo huo, Katibu Mkuu Msaidizi wizara ya elimu, sayansi na teknolojia Professa  Carolyne Nombo amesema Serikali ya Sweden ni mdau mkubwa katika elimu na kwamba kwa zaidi ya miaka 30 imekuwa ikitoa msaada mkubwa katika sekta ya elimu nchini.

Amesema mdahalo huo ni moja ya maboresho ya mfuko wa elimu ambao umekuwa ukifanywa chini ya wizara ya elimu yenye lengo la kuwawezesha wanafunzi kupata uzoefu dhidi ya wanafunzi wenzao nje ya nchi hususani Sweden ambao ni washirika wakubwa wa maendeleo nchini.

"Mdahalo wa leo wamejifunza Mambo mengi, yanayoendelea Tanzania lakini hata kule Sweden, ukiacha masomo lakini pia maisha ya kila siku ya wanafunzi," amesema.

Kwa upande wao Hans Masawe anayesoma sekondari Ilboru na Vicent Steven anayesema sekondari ya Kisimiri wote kidato Cha tani wanasema mdahalo huo umewasaidia kuweza kujua mazingira ya elimu nchini Sweden lakini pia kupata marafiki ambao wataendelea kubadilishana uzoefu wa kinasomo.

Awali akitambulisha mdahalo huo, Afisa programu anayeshughulikia elimu kutoka ubalozi wa Sweden nchini, Grimur Magnuson amesema programu hiyo inafanyika ikiwa ni muendelezo wa ubalozi kuwaunganisha wanafunzi wa Tanzania na sweden kuwajengea uwezo wa kimasomo wanafunzi wa nchi zote mbili.This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post