TIGO WAZINDUA PROMOSHENI MPYA " TEST ZALI USHINDE MILIONI 200"

 KAMPUNI inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania, leo imezindua promosheni mpya ya ‘Testi Zali’, ambapo Watanzania wataweza kujaribu bahati zao, kujishindia fedha kupitia bahati nasibu.

Promosheni hii itawawezesha wateja wa Tigo Tanzania kushinda kwa mara ya kwanza fedha nyingi zaidi ambapo mshindi kwenye droo kubwa ataondoka na sh. milioni 200, huku wengine wakijishindia fedha mbalimbali.

Wateja wanaweza kujisajili kupitia (SMS) na kushiriki mara kwa mara kwa ajili ya kushinda zawadi za pesa za papo hapo, pia kuingia kwenye droo kubwa ya bahati nasibu.
Testi Zali itatoa fursa kwa wateja kununua tiketi kwa urahisi na kuangalia kama wamejishindia zawadi ya fedha papo hapo na kujiongezea pointi za kuingia kwenye droo kubwa.

Promosheni hiyo inaanza leo Mei 24, 2021 na itaendelea hadi atakapopatikana mshindi wa sh. milioni 200 kwenye droo kubwa.

Tunatarajia kupata washindi 34,884 kila siku, kila wiki ambao watajishindia fedha zaidi ya sh. milioni 645.

Akizungumza jana katika uzindizi wa Promosheni hiyo, Mtaalamu wa Huduma za Kidijitali wa Tigo, Ikunda Ngowi, alisema: “Tumekuwa na ubunifu kila wakati, tumekuja na promosheni hii ya kusisimua ambayo itahusisha wateja wetu moja kwa moja na Tanzania kwa ujumla.

“Kwenye promosheni hii wateja watakuwa wakijiongezea pointi za kuingia katika droo kubwa ya bahati nasibu ya sh. milioni 200 ambayo ni ya kwanza nchini.

“Tunaamini itaongeza msisimko na tunatarajia kuwazawadia wateja wetu waaminifu hadi mwisho, ambao wanachangia ukuaji na mafanikio ya kampuni ya Tigo.”

“Kuna njia mbili za kuchagua washindi kuanzia sh. 1000 hadi sh. 500,000 ambazo zitakuwa zikitolewa kila siku, wakati sh. milioni moja, milioni 10 na milioni 20 zitatolewa kwa washindi wa droo ndogo,” alifafanua Ikunda.

Kushiriki katika promosheni hiii, mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15305, na kila ujumbe unatarajiwa kukatwa sh. 300.

Pia mteja anaweza kununua bando ya Testi Zali ya siku, wiki au mwezi kwa kupitia Tigo Pesa.

Katika promosheni ya Testi Zali, mteja anaweza kutuma ujumbe mfupi kwenda namba (15305), au kutumia menu ya Tigo (*147*00#), au (*148*00#).

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post