BALAA: WATU WAJIZOLEA MAMILIONI KUTOKA TIGO, PROMOSHENI YA SHEHEREKEA PESA NA TIGO PESA

 Na Mwandishi Wetu.

NI wiki ya nane sasa washindi wa wiki wa Promosheni ya Sherehekea Pesa, inayoendeshwa na Kampuni ya Mawasiliano - Tigo, jana wamejizolea zawadi zao.

Hadi sasa, Tigo imeshakabidhi, zawadi za jumla ya sh. milioni 80 kwa washindi 80 wa kila  wiki. 

Katika promosheni ya Sherehekea Pesa inayoendelea, washindi 10 hupatikana kila wiki, ambapo kiasi cha zaidi ya sh. milioni 200 zitatolewa kwa washindi wote watakaoibuka kidedea.

Promosheni ya Sherehekea Pesa ni sehemu ya sherehe ya miaka 10 ya kampeni ya Tigo Pesa nchini Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya kukabidhi fedha, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo, Mary Rutta, alisema ni wiki ya nane sasa wateja wa Tigo Pesa kutoka sehemu mbalimbali, wamezidi kujishindia pesa taslimu katika Promosheni ya  Sherehekea Pesa.

"Tunafanya droo hii kila wiki, washindi wanaibuka kidedea kwa kujishindia fedha taslimu.

“Pamoja na hayo, mteja wa Tigo anavyotumia Tigo Pesa kwa kulipa malipo ya bili, manunuzi ya bidhaa na huduma, kutuma pesa kwa wateja wengine wa Tigo Pesa, kupokea pesa kutoka benki, mitandao mingine na nchi zingine, ndivyo wanavyopata nafasi zaidi kushinda zawadi za pesa. ”  alisema Mary.

Alisema washindi wa fedha ya kila wiki, wanatoka katika mikoa mbalimbali wanaingia kwenye promosheni hiyo  ya kila wiki ambapo promosheni itaendelea kwa wiki mbili zaidi kutoka sasa na kila wiki washindi 10 watakabidhiwa zawadi zao.

Hadi sasa Tigo imetoa sh. milion 80 na imebakia sh. milion 120 kwaajili ya droo kubwa na washindi wa wiki, itakayofanyika Juni mwaka huu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post