VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUTOA ELIMU KUHUSU KURASIMISHA MALI

 


Na Mwandishi wetu


Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba amewaomba viongozi wa dini kutoa elimu kwa  jamii kuhusu umuhimu wa kurasimisha mali kwa lengo la kupunguza migogoro ya mali inayotokea, endapo itatokea mmoja wao amefariki au kuvunja uaminifu kwa mwenzake


Rai hiyo ameitoa mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya siku moja ya viongozi wa dini iliyoandaliwa na wakala wa Usajili Ufilisi na udhamini (RITA) kwa lengo la kushauriana jinsi ya kupata maamuzi ya pamoja.


Amesema kuwa, kumekua na migogoro mingi ya mali hasa kwa akina mama kutokana na watu kutorasimisha mali na shughuli zao wanazozifanya na kupeana vitu kwa kuaminiana hivyo wanakosa haki zao kwa sababu wamekosa kumbukumbu za mali zao.


"Watu wengi wanakosa kupata mali zao kwa kupeana nyumba, magari mashamba kwa kutumia uaminifu, endapo itatokea mmoja amevunja uaminifu ama amefariki yule ambae ana haki anaweza kufika hadi Mahakamani na akasa haki yake, kutokana na kukosa kumbukumbu inayomtambulisha yeye ndie mmiliki wa mali hiyo na kubaki kuishutumu amepokonywa haki Mahakama"amesema Mwigulu.


Aidha, amesema kuwa, mzazi anakua na malengo mazuri kwa mtoto wake, humtafutia mali kwa ajili ya maisha ya badae lakini kutokana na kutoandika kumbukumbu wanakwenda kurithi watu ambao hawakua kwenye malengo ya mali hizo navkuwaacha watoto kuteseka.


Kwa upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu (RITA) Emmy Hudson amesema amesema, lengo la semina hiyo ni kuwashirikisha katika kuwapa elimu kuhusu huduma wanazozitoa na  mabadiliko yanayofanyika katika huduma za sheria pamoja na kupata maoni yao yatakayoweza kuleta maendeleo chanya. 


Hata hivyo, amesema kupitia semina hiyo pia watakumbushwa wajibu wao kama viongozi wa dini katika kutekeleza majukumu yao kwa kufuata taratibu na sheria za usajili wa ndoa pamoja na wadhamini

 ili kuboresha mifumo yao na kukuza mahusiano na mawasialiano.


Hata hivyo, viongozi wa dini walioshiriki katika semina hiyo wamesema watahakikisha wanatoa maoni yao kwani migogoro ya ndoa imekua ni tatizo kubwa sana ndani ya jamii, hivyo kupitia semina hiyo wataweza kuleta mabadilioko huku wakiitaka Mahakama kuskiliza malalamiko ya pande zote mbili ndipo watoe hati za talaka. 


Aidha wameishukuru RITA kwa kuwashirikisha katika majadiliano hayo ambayo yatasaidia kupatikana kwa sheria nzuri zitakazoendana na mahitaji ya jamii ya kitanzania kuliko kuendelea kutumia sheria za nje ya nchi na zilizopita na wakati.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post