Redcross Arusha yapata viongozi wapya

Pichani ni Katibu Mkuu wa Taifa wa chama cha msalaba mwekundu Red cross Kejo akisoma matokeo ya uchaguzi kujaza nafasi zilizo wazi kwenye chama hicho mkoa wa Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha 

 Na Ahmed Mahmoud Arusha 

Chama Cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Arusha (red Cross society)kimefanya uchaguzi wa kuziba nafasi za uongozi ndani ya chama hicho

Nafasi hizo ni pamoja na mshauri wa mafunzo mshauri wa maafa na habari mshauri mipango na maendeleo mshauri wa jinsia na nafasi ya makamu mwenyekiti wa red Cross mkoa wa Arusha

Akiongoza uchaguzi huo katibu mkuu wa red Cross taifa  Julia's Kejo amewataka viongozi waliochaguliwa kutumia vyema nafasi zao katika kusaidia jamii kupata uduma ya kwanza 

Katibu amesema kwamba viongozi hao wanapaswa kusaidia pale majanga yanapo tokea pamoja na kuongeza wanachama wa red cross kuwa wengi kuimarisha chama hicho kufikia malengo ya kujiendesha chenyewe 


''Napenda kuona chama hiki kinafika mbali sana kwani Mkoa huu wa Arusha unaanzia herufi A hivyo mambo yote ya maendeleo katika chama hiki yanapaswa kuwa mbele hususani kuifikia jamii yenye uhitaji wa kupata huduma ya kwanza" alisema Katibu kejo ,,

Wakizungumza Mara baada ya kutangazwa kushinda nafasi zao viongozi waliochaguliwa wameleeza kufanya kazi na uongozi uliopo madarakani na kazi kubwa walionayo ni kuimarisha matawi katika Wilaya zote za Mkoa wa Arusha kuwa na nguvu ya kutoa huduma


Baadhi ya wajumbe wa (nec)wa chama hicho cha msalaba mwekundu akiwemo Doctar Christopher Nzella ambaye ni mhamasishaji mkuu wa chama  na felician  mtahengerwa  mjumbe na mwenyekiti wa mahafa red cross taifa kwa pamoja wamesema kwamba wanategemea kuona viongozi walio patikana wakiwa na maono ya kupambania chama katika kufikia malengo ya umoja kuanzia kazi ya tawi Wilaya Mkoa na taifa kukitangaza chama hicho.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Red Cross mkoa wa Arusha Dora Samson amewataka wajumbe na viongozi walio chaguliwa kuacha tofauti zao ikiwemo makundi ya kurudisha nyuma chama hicho na kuwa pamoja katika kusaidia jamii.

Amesema kabla ya uchaguzi huo kufanyika kumekuwepo na makundi ya wanachama kugawanyika kila moja kumuunga mkono mgombea wake hivyo ametoa rai kwa wanachama kuvunja makundi na kukijenga chama 

Makamu Mwenyekiti aliyechaguliwa Musa Luambano akiongea kwa niaba ya viongozi wenzake waliochaguliwa  ya amesema kwamba Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi na kuchaguliwa malengo ni kuhakikisha chama hicho kinakuwa na miradi yake inayojiendesha 

Uchaguzi huo umefanyika Mara baada ya nafasi kuachwa wazi na wajumbe wa red Cross katika mkoa wa Arusha Mara baada ya kukosa wagombea katika kipindi Cha nyuma ulipofanyika uchaguzi mkuu mwaka 2019.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post