Mfanyabiashara maarufu Arusha afariki dunia

Andrew George Mollel
a hisani ya gazeti la Mwananchi 


 Mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, Andrew Mollel ambaye alikuwa mwanzilishi  na Mkurugenzi wa kampuni mbalimbali mkoani Arusha amefariki dunia  na kuibua simanzi kwa wakazi wengi wa jiji hilo.

Akizungumza na Mwananchi leo, Februari 28, Mbunge wa jimbo la Monduli , Fredrick Lowassa amesema kifo cha Mollel  ni pigo kubwa katika jiji la Arusha kutokana na mchango wake.

Lowassa amesema taratibu za mazishi wa Mollel zinaendelea kufanywa na wanafamilia lakini, kubwa ambalo Arusha watamkumbuka ni kuandaa michoro ya mradi  mkubwa wa nyumba za PPF zilizopo eneo la Kijenge jijini hapa ambalo lilikuwa ni eneo lake.

Mollel alikuwa pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Happy Sausages ,Kijenge Animal Products Limited, Georges Center Ltd na AGM Holding  na pia mjumbe wa bodi mbali mbali hapa nchini.

Mollel pia alikuwa ni rafiki wa karibu wa Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.

Kifo cha mfanyabiashara huyu ni mfululizo wa vifo vya wafanyabiahara kadhaa katika jiji la Arusha katika siku za karibuni.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post