WAWILI WAUAWA NA JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA KWENYE MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI

 


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Salum Hamdun akiongea na wanahabari hawapo pichani mapema leo kwenye makao mkuu ya Jeshi hilo mkoani hapa.


Waandishi wa habari wakimfuatilia kamanda Hamdun alipokuwa akiongea nao mapema leo kuelezea kuuawa kwa Majambazi wawili pamoja na kukamatwa kwa watu tisa na Rushwa wakiwemo Askari wa Jeshi hilo 

Na Ahmed Mahmoud Arusha 

WATU wawili wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi wameuliwa usiku wa kumkia leo kwenye mapambano a kurushiana risasi na askari wa jeshi la polisi wakati walipokuwa wakijiandaa kwenda kupora kwenye duka la miamala la pesa .

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha,Salum Hamduni, amewataja waliofariki katika tukio hilo kuwa ni Joseph Bernad miaka 24  mkazi wa Sokoni one na mtuhumiwa mwingine ambao hajafahamika majina ake anae kadiriwa kuwa na miaka kati a 30 hadi 40  .

Amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 7.10 usiku wa kuamkia leo  eneo la Sakina kwa Idd jijini Arusha.

Amesema tukio hilo limetokea mara baada a mtuhumiwa aitwae Joseph Bernad,ambae amekuwa akihusika kwenye matukio mbalimbali ya unyang’anyi na uvunjaji wa nyumba  kukamatwa na pilisi na baada ya mahijiano alikiri kufanya mpango wa kwenda kuvamia duka na ndipo alienda na polisi kuwaonyesha watuhumiwa wengine na eneo ambalo kungelifanyika tukio hilo la uporaji .

Amesema polisi walipokaribia eneo la tukio walitumia mbinu a kumuachilia mtuhumiwa kwa lengo la kufanikisha ukamataji  lakini mtuhumiwa alikimbia na kutoa ishara kwa wenzake kuashiria kuna askari eneo hilo ndipo wenzake walipowafyatulia risasi polisi na askari hao walijibu mapigo mna kuwajeruhi mtuhumiwa huyo na mwenzake ambapo walifariki wakipelekwa hospitalini.

Amesema jeshi la polisi linaendelea kuwasaka waengine waliokimbia wakiwa na silaha moja Shortgun .

Amesema kwenye eneo la tukio kuliokotwa silaha mbili Bastola yenye risasi 4 ndani ya magazine na nyingine ikiwa na risasi tano ndani ya magazine

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post