Wanawake watengwa katika jamii kwa kudai umiliki wa ardhi

Mwandishi wetu,Arusha


Wanawake ambao wamekuwa wakipigania haki ya kumiliki ardhi yao, katika maeneo mbali mbali wilaya ya Ngorongoro mkoa wa Arusha, wamekuwa wakitengwa na jamii kwa kuonekana wanakiuka mila na desturi  licha ya serikali kuingilia kati na kuwapa haki zao.

Wakizungumza katikauchunguzi unaofanywa katika wilaya hiyo ,kwa kushirikiana na shirika la Hakiardhi, baadhi ya Wananchi, viongozi wa serikali na mashirika na kutetea haki za wanawake, wameeleza tatizo la wanawake kukosa haki ya kumiliki ardhi nikubwa katika wilaya hiyo.

Mkurugenzi wa shirika la Mimutie Women Organization(WMO),Rose Njilo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Arash, anasema hadi sasa wanawake kadhaa wamekuwa wakitengwa na jamii kutokana na kupambana kudai umiliki wa ardhi na kumtaja  Taleng'o Ole Sayeti mmoja wa wanawake katika kijiji hicho, aliyetengwa kutokana na kupinga kunyanyang'anywa ardhi.

"hivi sasa kwenye sherehe amekuwa haalikwi na mambo mengi ashirikishwi inaonekana kama mkosaji baada ya kupinga kunyanyaswa na kupokonywa ardhi hadi suala lake kulifikisha mahakamani na kupewa haki"amesema.

Njilo amesema licha ya jamii za kifugaji kuathirika na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi, ambalo limechangia mifugo kupungua na hivyo, kazi kubwa ya kulea familia kubaki kwa wanawake, lakini bado hawana haki ya kumiliki mali hata ambazo wamechangia kuzitafuta.

Mkurugenzi wa taasisi ya  Laretok -Le- Sheria  na haki  za binaadamu Ngorongoro, (LASHEHABINGO) Charles Ndangoya mkazi wa kijiji cha Wasso, Loliondo  wilayani Ngorongoro amesema ni muhimu jamii kutambua haki za wanawake kwani imekuwa ni changamoto ni kubwa na wamekuwa wakipokea malalamko mengi ya migogoro ya umiliki wa ardhi inayohusu wanawake na ambao wamekuwa wakidai haki hizo wamekuwa wakitengwa na kupigwa..

Hata hivyo, Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Rashid Taka amesema mifumo dume katika jamii na mila na tamaduni za jamii za kifugaji ni changamoto kubwa kuhusu haki za wanawake katika wilaya hiyo na ametaka jamii kubadilika na kutambua kila mtu ana haki ya kumiliki mali halali katika jamii.

Taka hata hivyo ameshauri kuwepo midahalo kuanzia ngazi za familia kujadili haki za wanawake na wanaume kuandika wosia mapema juu ya mgawanyo wa mali zao kwa kuwapa pia wanawake ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima katika jamii

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post