WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU HATARINI KUKUMBWA NA CORONA

 


Na Mwandishi Wetu, 
Arusha.

Wakati serikali ikitoa elimu juu ya kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (CORONA), kundi la watoto wa mitaani limesahaulika hali inayohatarisha afya na maisha yao.

Watoto hao hawana makazi maalumu kama ambayo mwandishi wa habari hii amewakuta wakizurura maeneo mbalimbali ya mjini wa Arusha na baadaye majira ya usiku kulala nje ya maduka ya wafanyabiasha katika ya mji huo hivyo ni muhimu sana kupatiwa elimu ya afya ya jinsi ya kujingika na ugonjwa huo.

Wakizungumza na APC Blog kwa masharti ya kutotajwa majina yao hali wala kupigwa picha baadhi ya watoto hao walisema hawajwahi kupatiwa elimu yoyote juu ya ugonjwa huo na kwamba wana uhitaji wa kujua jinsi ya kujikinga ili wasikumbane nao.

“Sisi tunaona watu wakipita katika maduka na huko standi kuwaelimisha juu ya Corona, lakini sisi hatujawahi kuitwa au kukusanywa mahali tukapewa elimu, naona ni kwa sababu hatuna makazi maalumu ya kuishi” Alisema Elias John ambaye siyo jina lake kamili.

“Kama unavyotuona hapa hatuna maski, ndoo za maji kwa ajili ya kunawa mikono, hatuna sabuni wala zile dawa za kujipaka mikononi (akimaanisha vitakasa mikono), kwa hiyo tunaiomba serikali itusaidie na sisi kwa sababu pia tunaishi mazingira hatarishi” Alisema Peter Godgfrey (siyo jina lake kamili)

Baadhi ya wafanyabiashara katika maeneo ya standi kuu walisema kuna umuhimu kwa kundi hilo kupatiwa elimu juu ya Corona kwani wamekuwa wakiishi maisha ya kawaida kama walivyokuwa wakiishi awali licha ya kuwepo kwa janga hili.

“Hata wewe hapa ulipo unaweza kuona wanavyopitapita, umeona hata mmoja amevaa barakoa?, hawajui lolote kuhusu kuchukua tahadhari, ni vyema idara inayowasimamia (Ustawi wa jamii) iwape elimu” Alisema mmoja wa wafanyabiashara ambaye hakutaka jina lake liandikwe.

Afisa Ustawi wa jamii jiji la Arusha alipotakiwa kuzungumza kuhusu suala hilo, alisema yeye siyo msemaji wa suala hilo licha ya mwandishi kumwambia Mkurugenzi wa jiji amemruhusu kulisemea lakini alisema anataka kibali cha maandishi kutoka kwa mkubwa wake wa kazi.

“Unajua dada haya mambo ya kupewa maelekezo kwa mdomo siyo sahihi, ningeomba nipate kimaandishi ili baadaye niwe salama, kwa kuwa kiutaratibu Mkurugenzi ndiye msemaji wa kila jambo linalohusu idara zote zilizopo ofisi ya halmashauri ya jiji” Alisema

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post