"SOS DAR IMETUSAIDIA BODABODA KUPUNGUZA UKATILI CHANIKA NA ZINGIZIWA"MAGAILA
Na Mwandishi wetu


Mwenyekiti wa Boda boda Kata ya Chanika Kwangwale, Saidi Magaila, amesema elimu waliopata kutoka Shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kuhudumia watoto ambao wamekosa malezi na walio katika hatari ya kukosa malezi (SOS) Children's Villages Dar es Salaam imeweza kuwasaidia kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia.


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika semina ya wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa mitaa, Dawati la kijinsia, vikundi vya kukopa na kulipa(Vikoba) pamoja na viongozi wa bodaboda iliondaliwa na Shirika hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.Amesema kuwa, wao kama boda boda kwa sasa wamekua mabalozi wazuri wa kuweza kupunguza vitenda vya ukatili katika maeneo ambayo wanaishi kwa kuhamasisha jamiii kuacha vitendo hivyo ikiwemo abiria wanaowapakia.


"Kabla SOS hawajafika hali ilikua mbaya Chanika na Zingiziwa kesi nyingi zilikua zinamaliziwa majumbani lakini tangu kilipoanzishwa kituo cha one stop center vitendo hivi vimepungua kwa kiasi kikubwa, tumeshawahi kumpeleka mama mmoja Polisi kwa kitendo cha kumnyanyasa mtoto kwa kumpiga na kumtumikisha kazi ambazo haziendani na umri wake"amesema Magaila.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kikundi cha Imarika Group, Husna Said amesema kuwa, watu wengi walikua na hofu ya kujiunga katika Vikoba vilivoanzishwa na SOS kwa kuhofia kufilisiwa lakini kwa sasa mwitikio umekua mkubwa kwani vimewawezesha kutimiza malengo yao.


Amesema kuwa, wameweza kupatiwa elimu ya uchumi jinsi ya kueka akiba, watu wengi wamenufaika sana ikiwemo kufungua biashara mbalimbali Kama vile migahawa na hata kuweza kumiliki ardhi kupitia Vikoba vyao."Kiukweli tulikua wamama wengi tunakosea kwenye suala la malezi ya mtoto lakini tulipopatiwa elimu ya biashara pamoja na malezi ya mtoto sasa tumenufaika watoto wamekua wawazi kwetu tunatenga mda wa kuzungumza nao kutuelezea yanayoeakabili"amesema Husna.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post