Makamanda wastaafu wa polisi wazuru kaburi la Hayati Moringe Sokoine

Kamanda wa  Mohammed Mpinga akiwa Katika boma la laibon,akiwa pamoja na watoto wa Laibon pamoja na wastaa6 wenzake wakiimba nyimbo za kiasili za kimasai walipotembelea boma hilo juzi lililopo Ndani ya Wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha (picha na Woinde Shizza ,ARUSHA)

Mkuu wa Wilaya Ya Monduli ACP Edward Balele  akiongea na Makamishna wastaafu wa  jeshi la polisi Nchini zaidi ya 34 walipofanya ziara ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko wilayani Monduli,lengo likiwa ni kuendelea kuhamasisha utalii wa ndani katika Wilaya ya hiyo na kuwa mabalozi wa vivutio hivyo katika wilaya hiyo (picha na Woinde Shizza , ARUSHA)

 Na Woinde Shizza ,ARUSHA

ZAIDI ya Makamishna wastaafu 34 wa  jeshi la polisi Nchini wamefanya ziara ya kutembelea vituo vya utalii vilivyoko wilayani Monduli,lengo likiwa ni kuendelea kuhamasisha utalii wa ndani katika Wilaya hiyo na kuwa mabalozi wa vivutio hivyo.

msafara ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Monduli ACP Edward BALELE, makamishna na maofisa wastaafu wa jeshi hilo  kutoka vitengo mbalimbali  wameitembelea  familia ya Waziri mkuu wa awamu ya kwanza marehemu  Moringe sokoine lengo likiwa ni kuzuru kaburi lake na kuishika mkono na kuyaenzi yale yote yaliyokuwa yakifanywa na kiongozi huyo enzi za uhai wake.

Aliyewahi kuwa kamanda wa kikosi cha usalama barabarani na RPC mkoa wa Mbeya  Mstaafu Mohammed Mpinga  alisema nia ya kufika Katika eneo  la kumbukumbu la kaburi la Marehem Moringe sokoine monduli juu  aliyefariki mwaka 1984 ikiwa ni miaka 36 Sasa kupita,  kumtambua sokoine kama shujaa aliyekua akiipambania Nchi kupitia nafasi iyo  kwakukemea wizi,ubadhilifu wa Mali ya umma, uzalendo,na  kuwa chachu kwa Taifa, kwani alikuwa ni mfano wa kuigwa  hasa kwa viongozi wengine na wameahidi kwenda kuyasimamia yale yote aliyoyatenda kipindi hicho.

Kwa  upande wake Kamishna msaidizi mwandamizi  mstaafu wa jeshi la polisi Tanzania Jamali Madenda alisema kupitia umoja huo wa wastaafu wa jeshi la polisi( TARPOA) ,wastaafu wanajivunia Nidhamu Bora ya utendaji na ufanisi uliotukuka  ndani ya jeshi pamoja na Serikali huku akitoa wito kwa viongozi waliopo madarakani kuwatumia Katika nyanja zote kwani Wana nguvu yakuyafanya yale yote watakayopatiwa kwa maslai mapana ya Nchi.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli ACP Edward Balele alisema anaamimi nguvu kubwa iliyotumika kutoka Kwa maofisa hao  wastaafu huku akieleza Serikali bado inawatambua na kuwathamini ivyo itaendelea kuwashika mkono licha ya kuwa ni hazina kubwa ndani ya Taifa,Katika masuala makubwa ya ushauri,na utendaji kazi endapo wataendelea kutumiwa watasaidia kuboresha jeshi ilo Katika nyanja mbalimbali.

Hata hivyo wastaafu hao wanaendelea na ziara yakutembelea Hifadhi mbalimbali ndani ya Wilaya ya monduli ikiwemo Jumuiya ya wanyamapori Randland,Manyara Ranchi , sambamba wamekabidhi madawati Katika Shule ya msingi Manyara,Nakuitembelea familia ya marehemu  Mzee Laiboni ktk kata ya Esilalei.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post