FAHAMU KWANINI Infinix NOTE 8 NI SIMU PENDWA KWA MWAKA HUU WA 2020
Toleo jipya la simu ya Infinix 8 Note iliyozinduliwa hivi karibuni imebeba processor aina ya Helio
G80 ikiwa ndio sifa kuu kwa simu hiyo na kupelekea kuvunja rekodi yake yenyewe kwa kuja na
simu janja yenye mfumo wa kukidhi mahitaji ya wadau wenye matumizi makubwa ya simu.
Infinix NOTE 8 imekuja na sifa nyengine zenye kuifanya simu hiyo kuwa ya kipekee kama vile
64MP Ultra HD 6, Battery mAh 5200, kioo cha nchi 6.95, Android 10.
Processor
MediaTek Helio G80 processor ikichagizwa na MediaTek HyperEngine Game Technology ambayo
inaipa nguvu simu hiyo na kuiwezesha kufanya kazi kwa haraka na kuhakikisha kuwa simu hiyo
inagusa maeneo mengine yote ya kimsingi kwa ufanisi. Chipset yenye sifa ya kufanya kazi vizuri
imefungwa katika simu hiyo si tu kuifanya iwe nyepesi wakati wa matumizi bali inaifanya kuwa
imara zaidi.
Inarahisisha games zinazochukua muda mrefu kufunguka kwa haraka na kucheza kwa ufanisi,
zinatumika katika maeneo maalum na games zenye ukubwa. Simu hii imeongezewa ufanisi wa
hali ya juu na maboresho ya uunganishwaji kwa minajili ya kuwezesha mtu kucheza game bila
bughudha.
Battery
Infinix NOTE 8 imebeba ujazo wa battery yenye mAh 5200M lengo ni kuona mtumiaji wa Infinix
Note 8 anaifurahiya simu yake kwa muda mrefu pasipo hofu ya kuzima chaji lakini pia hujaa
chaji kwa haraka. hii inapewa nguvu na teknolojia ya hali ya juu (power marathon) iliyomo
ndani ya simu janja ambayo hata kama chaji inakwisha inaiwezesha kutunza chaji kwa muda
fulani. Kwa wapenzi wa games, hii itawahakikishia wanakuwa na muda mrefu wa kucheza au
kutazama na Kwa mfanyabiashara au mjasiriamali aliyefanikiwa, Note 8 inakupa uhakika wa
haya yafuatayo kwa urahisi kama vile kutuma barua pepe, kutumia apps zinazohusu shughuli za
kiofisi, kutumia apps za kufanya mikutano kupitia video na mengine zaidi.
Vile vile simu hii ina teknolojia ya injini mbili. Jambo hili linaifanya Infinix Note 8 kuwa ya baridi,
ikipunguza joto kwa jotoridi 8 wakati inachajiwa.
Kamera
Moja ya sifa kubwa zinazoitofautisha simu hii na simu nyingine ni kuwa na kamera kubwa mbili
64MP Ultra HD 6nyuma na 16MP mbele. Kioo chake kikiwa na uwiano wa 20.5:9 ambacho kina
kamera ndogo mbili ambapo inakiwezesha kioo cha simu hiyo kuzunguka kufikia eneo la
kamera kiasi cha kutoleta usumbufu ukiitumia kuangalia video kwenye simu.
Simu hiyo yenye kioo chake cha kisasa (6.95" Dual Infinity-O Display) kinasaidia kamera
kuchukua picha zenye ubora kwa kuhakikisha hakuna vizuizi vyovyote vitakavyoharibu ubora wa
picha.

Infinix pia imepata suluhisho la kukabiliana na mazingira ya mwanga mdogo ambalo limekuwa
likiwasumbua watumiaji wakati wakichukua video. Kwa kutumia zaidi ya siku 180 (usiku na
mchana) kufanya utafiti na maboresho kukabiliana na suala hili, simu hii ina mfumo maalumu
wa kuiwezesha simu kufanya kazi katika mazingira ya giza (Note 8’s Ultra Night Mode 2.0)
inakupa matokeo mazuri katika mazingira yenye mwanga hafifu.
Muonekano
Muonekano wake utaweza kuwavutia watu mbalimbali na kwa namna simu hii ilivyo umuhimu
wake utaongezeka maradufu kama ambavyo ilivyo muhimu kwa mtu kuvaa nguo mwilini
mwake. Simu hii ina muundo mwepesi sambamba na GEM CUT ambayo imebuniwa kwa
kuangalia mitindo inavyokwenda na hadhi yake. Uumbaji wa simu hii ambao bado ni mfano wa
kuigwa umebebwa na mistari ya kipekee na uhalisia wa teknolojia. Muundo wake wa Gem Cut
ni mahususi kwa ajili ya kubadili muonekano wa mtumiaji.
Mapokezi
Ukipitapita madukani na kwenye mitandao ya kijamii utagundua ni simu iliyopokelewa vizuri
sana na hii ni huenda na wanachokipromoti ndicho wateja wanachokutana nacho baada ya
ununuzi, Infinix NOTE 8 imepokelewa vizuri na watu wa rika lote hasa wale wenye kuitumia
simu kama chombo muhimu katika shughuli za kila siku za kujipatia kipato.
Upatikanaji
Infinix NOTE 8 inapatikana kwa bei isiyozidi sh. 540,000 katika maduka yote ya simu nchini
Tanzania ikiwa na ofa ya GB 96 kutoka Vodacom lakini pia unaweza tembelea
https://www.infinixmobility.com/tz/ .

MAWASILIANO;
0744606222

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post