RAIS MAGUFULI AWATEUA PROF. KABUDI NA DKT. MPANGO KUWA MAWAZIRI.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13, 2020 amefanya uteuzi wa mawaziri 2 katika baraza jipya la mawaziri.

Kwanza amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Pili amemteua Dkt. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Mawaziri Wateule hao walikuwa wanashikilia nyadhifa hizo katika Baraza la Mawaziri liliopita na uteuzi huo unaanza leo Novemba 13, 2020.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post