WATU WATATU WAFARIKI KWA MLIPUKO WA GESI


Watu watatu wamefariki na wengine 28 kujeruhiwa jana nchini Thailand baada ya bomba la gesi kulipuka na kusababishia moto mkubwa mashariki mwa mji mkuu wa Bangkok.


Mlipuko huo uliharibu nyumba kadhaa na takriban magari 20 na pikipiki. Ilichukua zaidi ya saa moja kwa wazimamoto kuzima moto huo. Polisi bado hawajajua chanzo cha tukio hilo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post