UELEWA MDOGO WA JAMII WASABABISHA UGUMU WA UTENDAJI WA TAASISI BINAFSI

 

Mkurugenzi wa Me and Orphan Tanzania Musa Mofuga akimkabidhi mgeni rasmi Mhandisi David Mtunguja Cheti Cha kumtambua katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja wa Shirika hiloMkurugenzi na Mwanzilishi wa Shirika la Me and Orphan Tanzania ndugu Mussa Mofuga akizungumza katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja wa Shirika hiloBaadhi ya wanachama wa Shirika la Me and Orphan Tanzania wakiwa katika Hafla ya kutimiza mwaka mmoja wa Shirika hilo lenye makao take makuu Jijini ArushaBaadhi ya Wageni waalikwa katika hafla hiyo  wakifuarahia Jambo  Baadhi ya wenyeviti wa Taasisi binafsi walioshiriki katika hafla hiyo ya kutimiza mwaka mmoja kwa Shirika la Me and Orphan Tanzania lenye makao yake makuu Jijini Arusha


Na.Vero Ignatus,Arusha

Uelewa mdogo wa jamii katika huduma za Mashirika yasiyo ya Kiserikali, imepelekea kuleta ugumu na kutoonyesha ushirikiano katika utendaji kazi, katika kufikia malengo yao kama inavyotakiwa

Musa William Mofuga ni mwanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali linaloitwa  Me and Orphans Tanzania, lenye makao makuu yake mkoani Arusha, anasema lengo kuu la shirika hilo ni kupata jamii yenye huruma ,utu kwa watoto yatima, na watoto wa mitaani, katika kuwapatia malazi,elimu na masuala ya afya

Alisema Taasisi hiyo inashirikiana na serikali kuibua changamoto zilizopo katika jamiii,na kusaidia kupata tarifa muhimu ambazo wakati mwingine zinakuwa hazijasikika mahali pengine .ili kuzipatia ufumbuzi na kuziwasilisha kwenywe vyombo vinavyohusika kwaajili ya utatuli zaidi.

Mofuga alisema kuwa  dhamira yao kuu ni kuwasaidia watoto yatima katika jamiii ,kwa kupitia kutoa elimu kwa jamiii, na kwa michango ya wadau wa maendeleo ya jamii, ili watoto yatima waweze kupata mahitaji ya msingi na kuhakikisha usalama wao. 

Alisema kuwa wanasaidia kuibua chamgamoto zilizopo ndani ya jamii, zinazochangiwa na mila nadesturi mbaya, ambazo ni kandamizi kwa kutoa elimu kwa kupitia warsha,semina na vyombo vya habari walau kupunguza changamoto hizo

 Aidha mwanzilishi wa shirika hilo alisema changamoto kubwa wanazokabiliana nazo kwa sasa  ni kukosa pesa za kutosha, na kupelekea kuelekeza nguvu kubwa kwa michango ya ada za wananchama, na viongozi jambo ambalo halijaweza kufanikiwa kwa asilimia kubwa

Hivyo basi  Kutokana na hali hiyo imepelekea shirika hilo kukosa ofisi yake ya kujitegemea ,na kuwalazimu kutumia ofisi ya kampuni fulani ambayo waliiazima kwa muda ,na kila kitu kilichomo kwenye ofisi hiyo kinakodishwa na ada yake ni kubwa.

Aidha ameiomba jamii kutambua kuwa uwepo wa mashirika hayo binafsi, lengo  kubwa ni kushirikiana na serikali  kuibua changamoto mbalimbali za kijamii na kuzitafutia ufumbuzi,kuhakikisha kuwa jamiii inapata unafuu katika changamoto hizo,kwahi serikali peke yake haiwezi kutekeleza mambo yote

Ameainisha shauku yake kwa kusema kuwa kwa uongozi utakaoingia madarakani ujitahidi kuwa karibu na taasisi hizo binafsi, kwani zinafanya kazi kubwa za kuibua changamoto ndani ya jamii,lakini wanapopata changamoto katika utendaji kazi wao,hawana mahali sahihi pa kupata majibu ya maswali yao,na hiyo ni  kutokana na kutokuwa na uwazi baina ya mashirika ya siyo ya kiserikali na uongozi unaokuwa madarakani

 Amesema kuwa shirika hilo lenye wanachama hai wapatao 36 kutoka mikoa mbalimbali nchini , ndiyo wanaojitolea kwa kiasi kikubwa katika mapato ya ndani ya sughuli za shirika hilo, ambapo wameweza kutoa misaada ya vyakula,mavazi,na kudhamini baadhi ya watoto, katika maeneo ya Arusha mjini kata ya Elerai ,wilaya ya Arumeru,wilaya ya ngorongoro,Oldonyosambu mtaa wa namelok na mtaa wa Oldonyowasi

Shirika hilo la Me and Orphan Tanzania limesajiliwa kiserikali kwa namba 00NGO/R/00361,ambapo wana jumla ya watoto yatima 20 waliopokatika shirika hilo kwenye kituo chao kulichopo Oldonyosambu Mkoani Arusha.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post