Uchumi wa Marekani umeshuka kwa asilimia 32.9 kutokana na janga la Corona, ikiwa ni pigo kwa rais Donald Trump kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.

 Mwandishi wetu na Mashirika ya Kimataifa

Kushuka kwa uchumi nchini Marekani kumeshuhudiwa kati ya mwezi Aprili na Juni, kwa mujibu wa watalaam wa masuala ya uchumi, katika kipindi ambacho nchi hiyo imekuwa ikishuhudiwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona.

 

Mwezi Aprili pekee, zaidi ya ajira Milioni 20 zilipotea nchini humo, baada ya biashara nyingi kufungwa na watu kusalia nyumbani kutokana na janga la Corona ikiwa ni kutekeleza agizo la mamlaka wa kiserikali nchini humo.

 

Wiki iliyopita pekee, watu Milioni Moja na Laki nne waliripoti kupoteza ajira katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa duniani, wakati huu wachambuzi wakibashiri kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi katika siku zijazo kabla ya uchumi kuanza tena kuimarika taratibu.

 

Wanasaisa wa chama cha Republican na Democratic, wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusu namna ya kuimarisha tena uchumi wa taifa hilo kutokana na janga la Corona wakati huu taifa hilo likielelea kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Nevemba.

 

Wakati hali hii ikionekana kuathiri maelfu ya wananchi katika nchi ya Marekani, nchi za Afrika hali ni tete baada ya ugonjwa huo unaozuia madhara katika fumo wa hali ya hewa kuendelea kuua watu wengi Zaidi.

 

Hali hiyo imekuwa tishio kubwa la kuibuka kwa tatizo la njaa kutokana na nchi nyingi wananchi wake kushindwa kuzalisha baada ya kutakiwa kukaa ndani na nchi zao ikiwa ni njia ambazo wamekuwa kuzifuata ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

 

Nchini Tanzania wananchi wameendelea kufanyakazi za uzalishaji kama kawaida baada ya Serikali yake kukataa kuzuia shughuli za uchumi kutoendelea kwa kuwafungia ndani wananchi wake jambo ambalo limeendelea kupongezwa na wananchi mbalimbali.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post