Mawakala wa vyama vya siasa waapishwa Arusha

 Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini limewaapisha mawakala wa Uchaguzi wa vyama 15 vya siasa vilivyo ingia katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu utakao husisha uchaguzi wa viongozi ngazi za udiwani,ubunge na urais.


Akiongea wakati wa mawakala hao kula kiapo Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini Dk John Pima,amesema miongoni mwa mawakala waliyo kuwa wanatarajiwa kula kiapo hicho nimawakala ni 11,833, Lakini hadi kufikia siku ya kiapo waliyo thibitishwa ni 11,311 pekee.


"Tarehe 15 Octoba 2020 nilitoa taarifa kwa vyama vya siasa kuwakilisha majina ya mawakala wao wanaotarajia kusimamia zoezi la Uchaguzi katika kila kituo tulipokea idadi ya Jumla ya Mawakala 11,833 lakini hadi kufikia leo kama inavyo onyesha kwenye ratiba yetu ya Tume ya uchaguzi ni siku ya kuapisha mawakala tuna Jumla ya idadi ya Mawakala 11,311 tu na ndiyo waliyothibitisha na kuapisha". Alisema Dkt Pima.

IMG-20201021-WA0200


Aidha Dk John Pima alieleza mbali na kupokea barua za uthibitisho za Mawakala 11,311 lakini bado kulikuwa na mapungufu baada ya kupokea barua hizo walibani kuwa barua zilikuwa na mapungufu ya ukosewaji majina ya vituo vya usimamizi katika kata husika,barua kutosainiwa na katibu wa chama husika,nakala za vitambulisho,kutumika mihuri zaidi ya mmoja katika barua za sehemu moja,Pamoja na mawakala kutambulishwa na makatibu wa jimbo badala ya wilaya.


"Vyama vyote 15 leo tumeviita na kuwapa mapungufu hayo yote na vingine vimesha fanyiwa marekebisho na wengine tumewapa muda wa kufanya marekebisho ili waweze kukidhi vigezo na kuapishwa ili waendelee na utaratibu mwingine". Alisema Dkt Pima.

IMG-20201021-WA0201


Pia Dkt Pima aliweza kutoa wito kwa mawakala wa vyama vyote kuzingatia maelekezo yaliyo tolewa na Tume ya Taifa ya Uchanguzi kama sheria,kanuni,miiko na taratibu za kuzifuata katika zoezi zima la uchaguzi.


"Mbali na wito wangu kwa mawakala wa usimamizi wa uchaguzi natoa wito pia kwa wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini kuwa watulivu na kuwa tayari kwa zoezi la upigaji kura na nina wahakikishia maandalizi ya uchaguzi yameenda vizuri  yatakayo mfanya mwananchi wa Arusha kupiga kura kwa utulivu siku ya tarehe 28 Octoba 2020 katika kituo chake alicho jiandikisha ili aweze kumchagua kiongozi anaye mtaka na kutimiza wajibu wake kikatiba". Alisema Dkt Pima.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post