ITEL WAZINDUA SIMU MPYA ITEL S16

 


Kampuni ya Simu ya ITEL imeitambulisha simu yake aina ya ITEL S16 ambayo ina kamera tatu upande wa nyuma pamoja na mbele na inasifika kwa kukaa na chaji kwa muda mrefu.


Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, Afisa uhusiano wa Kampuni ya ITEL Bw.Fernando Wolle amesema kuwa simu aina ya ITEL S16 ni kubwa na ina AI kamera tatu kwa nyuma na mbele pia ni AI selfie Camera na kikubwa upande wa betri ni 4000mAh.


Amesema simu hiyo kwasasa inapatikana Tanzania nzima kwenye maduka ya simu kwa bei nafuu yaani kuanzia laki moja na sitini mpaka laki moja na themanini (160,000/= hadi 180,000/=).Aidha amesema kuwa kuna kampeni ya selfie Tanzania nzima kwa upande wa Dar es Salaam,Mbeya, Arusha na Mwanza ambayo ni maalumu kwa wateja wao na wale wote watakaotembelea katika maduka ya simu.


“Mtu anaweza kupiga picha kwa kutumia muonekano wa nyuma Mlima Kilimanjaro,Wanyama pamoja na simu yenyewe ITEL S16 na kuweza kushare kwenye social media na anaweza kujishindia simu S16”. Amesema Bw.Wolle.Pamoja hayo Bw.Wolle amesema kuwa simu hiyo inakwenda na kampeni ya Ukinunua simu moja, Shilingi elfu moja (1,000/=) ya pesa uliyonunulia simu inakwenda kwa watoto yatima na ni kampeni ya mwezi mmoja. Kampeni ikishaisha wataweza kupeleka msaada huo wa fedha iliyopatikana kwenye kituo cha watoto yatima.


Hata hivyo Bw.Wolle amesema kampuni ya ITEL inapenda kuwahamisha wateja wanaotumia simu za batani kwenda katika ulimwengu wa kidigitali kwani simu zao ni bora zenye bei nafuu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post