PINDA azindua kampeni za CCM Arumeru Magharibi

 *UZINDUZI WA KAMPENI CCM ARUMERU MAGHARIBI 

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akizindua kampeni za CCM Arumeru Magharibi
Na Mwandishi Wetu, Arumeru

Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa ambae pia ni waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe, Mizengo Pinda leo 19/09/2020  amezindua kampeni za ubunge wa jimbo la Arumeru Magharibi.

Akimnadi mgombea wa jimbo hilo, Noah Lembrusi Seputu* , Mhe Pinda amesema jimbo la Arumeru Magharibi kwa muda mrefu limekosa mwakilishi sahihi wa kuwasaidia wananchi na kuwataka wananchi wa Arumeru Magharibi kumchagua Ndugu Noah Lembrusi Seputu kutoka chama cha mapinduzi CCM akawasemee Bungeni ili jimbo liweze kunufaika zaidi na miradi ya Maendeleo.

Jimbo la Arumeru kwa miaka mitano iliyoisha lilikuwa likiongozwa na mbunge kutoka  Chama Cha demokrasia na Maendeleo Chadema Gibson Meiseyeki ambae kwa Mara nyingine na yeye amepitishwa na Chadema kuwania nafasi hiyo.

Jumatatu Tarehe 21/09/2020 chama cha mapinduzi wilaya ya kichama ya Meru inatarajia kuzindua kampeni za uchaguzi jimbo la Arumeru Mashariki.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post