Mgombea ubunge wa Tadea aahidi kuwashinda Lema na Gambo

 

 Na Woinde Shizza,  Arusha 

Mgombea ubunge Jimbo la Arusha mjini  kupitia Chama Cha ADA TADEA Zuber Mwinyi ameaidi kunyakua ubungrJubunge katika jimbilo la Arusha Mjini na kuwashinda wagombea wengine ambao Ni Godbless Lema mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Pamoja na Mgombea ubunge wa  CCM,Mrisho Gambo kwani yeye Ni kiongozi makini aliejipanga kuleta Maendeleo ndani ya Jimbo hilo

Ameyasema hayo Jana wakati wa uzinduzi wa kampeni wa Chama hicho ambao uliofanyika katika viwanja vya standi kubwa ya mabasi ya  mkoani Arusha ambapo Alisema kuwa yeye ni mgombea tofauti na wengine kwani yeye hagawi fedha kwa wananchi  ili wamchague bali anawaambia wananchi nini atawafanyia pindi wanapomchagua.

Amesema kuwa iwapo wananchi wa Jimbo la Arusha mjini wakimchagua atahakikisha anasimamia rasilimali zote za Jimbo la Arusha mjini ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote .

Aidha Amesema kuwa atahakikisha wafanyabiashara wote wanakuwa marafiki na TRA kwa  kuhakikisha wanakadiriwa Kodi zenye viwango vinavyoendana na biashara zao ,ambapo Alisema kuwa atatengeneza mpango maalum wa kurudisha biashara zote zilizofugwa  na hatakaa kila Mara na wafanyabiashara ili kupata njia rahisi na nzuri za kuendeleza biashara zao

Kwa upande wa bodaboda Alisema kuwa anampango wa kutengeneza mpango mkakati wa Vijana wa usafirishaji ili waweze kupata mikopo ya bajaji na Toyo kwa Bei nafuu na bila riba .

Aliongeza kuwa atahakikisha wamama wote wajawazito wanapoenda kujifungua hawalipishwi kitu chochote kile pale wanapoingia hospitali Hadi pale wanaporuhusiwa kurudi majumbani mwao.

"Kwakuwa elimu Ni kila kitu nitaweka kitengo maalum Cha kusaidia mikopo ya wanafunzi  iweze kupatikana kwa wakati Ndani ya Jimbo letu na kwakuwa elimu ni bure nitahakikisha kila mtoto anaeanza shule mzazi wake hawalipishwi mchango wowote ule na nitaakikisha madarasa yanajengwa ya kutosha na madawati yanakuwa ya kutosha kulingana na idadi ya wanafunzi"Alisema Zuber

Aliwataka wananchi kuchagua viongozi watakao badilisha maisha yao na wasichague viongozi kwa kuhamasishwa na vyama.

Picha ikionyesha wa kwanza kulia ni mgombea Ubunge Jimbo la Arusha mjini Kupitia Chama Cha ADA TADEA , katikati Godbless Lema kutoka CHADEMA Pamoja na Mrisho Gambo kutoka Chama Cha mapinduzi wote wakiwa ni wagombea ubunge katika Jimbo la Arusha mjini

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post