DKT. BASHIRU ATOA ONYO KALI KWA WANAOKUSANYA SHAHADA ZA KUPIGIA KURA KWA VISINGIZIO VYA KUTOA MIKOPO KWA WANANCHI

 


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally ametoa onyo kali kwa wale wote wanaopita kukusanya shahada za kupigia kura kwa visingizio vya kutoa mikopo kwa wananchi. 


Dkt. Bashiru ameyasema hayo jana Septemba 27, 2020 katika kata ya Engusero akielekea Kiteto na Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania kwa tiketi ya, CCM, Mama Samia Suluhu.


"Shahada ya kupigia kura inakazi ya kupiga kura. Tusidanganywe kuwa shahada yako inaweza kukufanya kupata mkopo.


" Ukiona mtu anakumbai (lete shahada ya kupigia kura upate mkopo) mtafute Mwenyekiti wa Kijiji au Kitongoji akamatwe kwani anavunja sheria" alisema Dkt. Bashiru.


Ameongezea kwa kusema "Pia ukiona mtu anakuhamasisha kufanya fujo, usikubali kwa sababu nchini hii ni uhuru na kisiwa cha Amani".

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post