WATUMBULIWA NA NAIBU WAZIRI YA MAJI20200805_175652

NAIBU  waziri  wa maji Jumaa Aweso  ametumbua  meneja wa maji mkoa wa  Iringa Mhandisi  Shaban Gelen  pamoja na meneja wa maji  wilaya ya  Mufindi mhandisi Robart Mgombela  kutokana na uzembe  wa  ucheleweshaji  wa utekelezaji  wa  maradi wa maji Sawala na Nyololo wilayani Mufindi  pamoja na  serikali  kutuma  pesa  za utekelezaji wa miradi hiyo.

Aweso  alisema  kuwa  wakati Rais Dkt Johm Magufuli  akiwaapisha baada ya  kuwateua  aliwaeleza mambo mawili  likiwemo la  kuwa  ninawateua nendeni mkafanye kazi  ya  kuwatumikia  wananchi na msipo  fanya kazi niliyowatuma  nitawatumbueni   hivyo kabla ya  Rais  hajamtumbua kwa  kushindwa  kuwatumikia  wananchi ameona  awatumbue  hao wasaidizi wake kwa kukwamisha  utekelezaji wa miradi ya wananchi .

Kwani alisema  kuwa  miradi hiyo ya maji ni miradi ya  muda mwingi na ahadi ya Rais  ni  kuona wananchi  wanapata  huduma ya maji ndani ya mwezi  wa nane  ila  watendaji hao kwa  uzembe  wamechelewesha  ukamilishaji  wa miradi hiyo na ule wa Sawala pamoja na kukamilika ila  mhadisi wa  wilaya alipewa  fedha  kwa ajili ya ukarabati wa  tenki la maji ili wananchi  waweze  kupata maji safi na salama  lakini ameshindwa  kutekeleza na hadi  sasa tenki hilo  halina  mfuniko  wa  kuzuia uchafuzi wa  maji pamoja na fedha kuwepo .

Akizungumza jana  baada ya  kukagua  maendeleo ya  miradi hiyo ya maji katika mkoa wa Iringa Aweso  alisema  kuwa  amefurahishwa  nusu na utekelezaji wa miradi  hiyo ila  nusu hajafurahishwa na anaona ni lazima   kuchukua hatua  ya haraka ya  kuwapumzisha  watendaji  hao wakuu wa maji katika  mkoa wa Iringa na wilaya ya  Mufindi  ili  kuwapata  watu ambao  watafanya kazi kulingana na matakwa ya  serikali ya  kuharakisha huduma ya maji kwa  wananchi  huku  hao  ambao walikuwepo katika nafasi  hizo za juu  watapangiwa  kazi nyingine za  kufanya na sio nafasi walizokuwa nazo.

"  Wananchi  wetu  wanahitaji kuona wanapata  huduma ya maji na  sio kuona  wanaendelea  kupata maneno kutoka kwa  watendaji wa  serikali  ila bado wataalam   wamegeuka kuwa wana siasa kwa  kutoa maneno zaidi badala ya  vitendo  hivyo nataka  meneja  wa maji mkoa wa Iringa atueleze  lini mradi huu utakamilika na kwanini amechelewesha  na kuifanya  serikali kutoaminika kwa wananchi "  alisema Aweso 

Kuwa serikali ya awamu ya tano  chini ya Rais Dkt Magufuli ni serikali ya  kazi zaidi na sio maneno  hivyo hawezi  kuona wataalamu hao wakiendelea  kupiga maneno  wakati  wananchi  wanakosa  huduma ya maji   hivyo njia  sahihi ni  wataalamu  hao kupisha pendembe  ili  kuweka watendaji watakaowajibika kwa  wananchi kuona  wanapata  huduma ya maji  safi na  salama .

Pamoja na  kuwatumbua  mameneja hao  Aweso  alipongeza  mradi wa maji wa Ilula  kuwa umetekelezwa  vizuri na  kuwatumia  salumu  mameneja wa maji  wilaya  na mikoa nchini  kuwa katika  ziara  yake hiyo hatawafumbia macho na  serikali hapo tayari  kuadhibiwa na wananchi kwa  kushindwa  kutekeleza ahadi yake ya maji kuwa kabla ya  wananchi hawajaiwajibisha serikali  wao  watakuwa  wamewajibishwa .

Akizugumza kwa niba ya meneja wa maji  wilaya ya Mufindi  ,meneja wa mkoa wa Iringa Mhandisi Shabani  pamoja na  kuomba radhi  wananchi kwa  uzembe  uliojitokeza aliomba kupewa muda hadi mwezi ujao ili  mradi  wa maji Nyololo  uweze  kukamilika pamoja na kuwa mradi huo hakuna shughuli iliyoanza kutekelezwa kama ya uchimbaji mitaro na usogezaji wa tofali  pamoja na vifaa vya kuunganishia maji hayo

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post