WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WATAKIWA KUONGEZA JITIHADA KATIKA KUENDELEA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO.

 #Repost @wizara_afyatzNa WAMJW- Moshi, KILIMANJARO 


MGANGA Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameagiza ndani ya miezi sita (6) Wakurugenzi wa Hospitali, Waganga Wakuu wa mikoa, Waganga Wakuu wa Wilaya na Waganga wafawidhi wote nchini kuongeza kasi katika kuendelea kupunguza zaidi vifo vya mama na mtoto kwa kuboresha huduma na usimamizi katika maeneo yao. 


Mganga Mkuu wa Serikali ametoa agizo hilo wakati akiongea na Watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro_ Mawenzi kwenye ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma na ujenzi wa miundombinu ya afya katika Mkoa huo Kilimanjaro.


"Wakurugenzi wakuu wa Hospitali Taifa, Kanda, Waganga Wakuu wote wa Mikoa, Wilaya pamoja na Waganga Wafawidhi wa Hospitali zote mlifanyie kazi hili suala la kuendelea kupunguza zaidi vifo vya akina mama wajawazito, na nawapa miezi mitatu hadi sita, nione hali ya vifo vinaendelea kushuka zaidi kila Kanda, Mkoa, Wilaya, na Vituo vya afya.  Baada ya miezi sita Serikali chini ya Wizara za AFYA na TAMISEMI tutafanya tathimini ya utendaji wenu kuhusu hili swala na viashiria vingine vya matokeo ya uwajibikaji wenu. 


Aliendelea, Mshirikiane kuunda vikosi kazi ambavyo vitaongeza kasi ya kuendelea kupunguza vifo vya watoto wachanga na mama katika Hospitali zetu na vituo vya afya, huku akiweka wazi kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya, huku akisisitiza kuwa, uwekezaji huo hauendani kabisa na hali ya vifo vya akina mama na watoto uliopo kwa sasa.


Aidha, Prof. Makubi amesema kuwa, vifo vya akina mama wajawazito na mtoto vinaweza kupungua mno nchini kama kutakuwa na uwajibikaji na kujitoa kwa kila mtu kwa nafasi yake, ikiwemo uratibu mzuri baina ya watoa huduma za afya ili kuondoa ucheleweshaji wa kupata huduma kwa mama wajawazito, huku akisisitiza kuzitumia Hospitali ya taifa na za Kanda ili kubadilishana ujuzi na hospitali za ngazi ya chini na  utambuzi wa viashiria vibaya kwa mjamzito wakati wa mahudhurio ya  kliniki...

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post