VIRUSI VYA CORONA; MARUFUKU KUTEMBEA MAJUMBANI KATIKA BAADHI YA MAENEO UINGEREZA

People in masks dining out

Mamilioni ya watu kaskazini mwa Uingereza wanakabiliana na sheria mpya ya marufuku ya kutembeleana majumbani kufuatia ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Sheria hiyo imeanza kutekelezwa mijini Manchester, mashariki ya Lancashire na sehemu ya magharibi mwa Yorkshire.

Katibu wa wizara ya afya ameiambia BBC kuhusu ongezeko la maambukizi kutokana na tabia ya watu kutembelea marafiki na ndugu.

Baadhi wamekosoa muda ambao tangazo hilo lilitangazwa kuwa majira ya jioni ya Alhamisi.

Katibu wa wizara ya afya bwana Matt Hancock alisema taarifa hiyo ililenga watu ambao walikuwa wamekutana na waliombukizwa kuacha kutembelea jamaa zao ili kupunguza maambukizi.

People having dinner at home

Marufuku mpya ambayo imeanza usiku wa kuamkia leo saa sita, ina maanisha kuwa watu hawataweza kutembeleana majumbani au katika bustani binafsi.

Vivyo hivyo wamesitisha watu kujichanganya kwenye vilabu vya pombe, migahawa ingawa wataweza kutembelea maeneo ya hosptali.

Mabadiliko hayo yamekuja wakati wa maandalizi ya sherehe za Eid na wiki chache tu baada ya Uingereza kulegeza masharti yakei ya kuwaruhusu watu kukutana nje tangu mwishoni mwa mwezi Machi.

Sheria hiyohiyo imewekwa Leicester, eneo ambalo kuna marufuku tangu mwezi uliopita.

Ingawa vilabu ,migahawa na maeneo mengine yanafunguliwa mjini kuanzia Jumatatu.#chanzo BBC

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post