TECNO YATARAJIA KUANZA KAMPENI KUBWA YA "VIMBA SEASON"

Na Mwandishi Wetu

Habari za ndani kutoka TECNO zimebainisha kuwa kutakuwa na kampeni maalum ya Vimba Season ambapo mteja atakayenunua TECNO CAMON15 na Spark5 ataweza kujinyakulia zawadi za papo kwa papo na kupata nafasi ya kuingia katika droo ya zawadi kubwa ya kushindania gari kali itakayotolewa na TECNO kwa wateja wake.
TECNO kwa kushirikiana na Dstv wameandaa pia zawadi nyingine nyingi kwa wateja wa TECNO CAMON 15 na Spark5 ambapo kwa mteja atakayenunua moja ya simu hizo ataweza kuibuka na zawadi ya king’amuzi cha Dstv pamoja na dishi lake kilicholipiwa tayari chaneli katika kifurushi cha familia kwa muda wa mwezi mmoja.

           
                                                
TECNO CAMON 15 na Mwonekano wa Zawadi ikiwemo Gari na seti ya King’amuzi cha Dstv
Akizungumza nasi mmoja wa wafanyakazi wa TECNO alithibitisha kuwepo kwa kampeni hiyo pamoja na zawadi hizo na kuongeza kwamba wamedhamiria kutoa zawadi nyingi na kubwa ikiwemo zawadi ya gari katika kipindi hiki huku lengo kubwa likiwa ni kuwajali wateja wao.
“Ni kweli kutakuwa na kampeni ya mwezi mzima ya ‘Vimba Season’ ambayo safari hii tumeshirikiana na Dstv, kwahiyo mteja atakayenunua TECNO Camon15 au Spark5 kwanza atapata zawadi za papo hapo kama vile seti ya king’amuzi cha Dstv bure kilicholipiwa tayari katika chaneli za kifurushi cha familia kwa mwezi mzima na zawadi nyingine, pia mteja atapata nafasi ya kuingia kwenye droo kubwa ya kushindania gari nzuri itakayotolewa kwa mshindi baada ya kumalizika kwa kampeni hii.”Alisema mfanyakazi wa TECNO.
                                                                                         
                             
                         
Baadhi ya zawadi nyingine kama zilivyoshikwa na Msimamizi wa duka la TECNO.

Kampeni hiyo ya Vimba Season imethibitishwa kuwa itazinduliwa na TECNO mapema mwezi huu huku ikitarajiwa kufanyika nchi nzima katika maduka makubwa ya TECNO yaani ‘Smarthubs’ kwa muda wa mwezi mmoja.
Je, ungependa kufahamu zaidi kuhusu kampeni hii ya ‘Vimba Season’, kutoka TECNO?  Tembelea kurasa za TECNO; Facebook, Instagram na Twitter 

https://bit.ly/2XsrPWm

@tecnomobiletanzania.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post