SERIKALI YASISITIZA UTENGENEZAJI MIUNDOMBINU YA MAJI, DC ATOA SIKU SABA

Na Mwandishi wetu Tarime

Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhandisi Mtemi Msafiri ametoa muda wa siku saba kwa  wakala wa Huduma za maji safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA kumalizia miradi yote ya maji pamoja na utengenezaji wa visima vyote.

Mkuu wa Wilaya alitoa kauli hiyo kipindi akifungua kikao cha wadau ambao ni watumiaji wa maji Mjini na Vijijini kilichofanyika chuo cha ualimu TTC Mjini Tarime.

Mkuu  wa wilaya alisema kuwa wafanyakazi wote kutoka mamlaka hiyo sasa watoke ofisini kwa ajili ya kumalizia miradi yote ya maji ili wananchi waendelee kunufaika na siyo kulalmika kila muda.

“Maji ni Muhimu sana siyo kama umeme kuwa utatumia sola au utawasha mshumaha pia serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maji kuna visima mpaka sasa havifanyi kazi kwa sababu ya vifaa ambavyo vinagharama ndogo hatuwezi kwenda hivyo pia kuna vifaa vinapaswa kufuatwa Dodoma mfano Paip

Wadau wa maji wakiwa katika kikao hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime mhandisi Mtemi Msafiri akiongea na wadau wa maji katika kikao kilichofanyika ukumbi wa chuo cha ualimu TTC Mjini Tarime.
u sasa hatutaki kujua hilo tunataka maji”  alisema Mkuu wa Wilaya.

 Mtemi alisisitiza kuwa wakandarasi wote wanaotekeleza miradai ya maji wilayani humo kukaa maeneo ya kazi ili kukamilisha mapema miradi hiyo huku akitolea mfano mradi wa maji Gamasara unaodaiwa kufanya kazi kwa wiki mbili na kisha kusimama.

“Nasikia mkandarasi aliyetengeneza mradi wa maji Gamasara mjini Tarime anazunguka Dodoma tu na mradi wake umefanya kazi wiki mbili na sasa umesimama nakuagiza wewe msimamizi wa maji RUWASA mpigie simu arudi kazini mara moja” alisema Mtemi.

 Mhandisi Marwa Mulaza ni Kaimu Meneja wa wakala wa Huduma za maji safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA alisema kuwa serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya upatikanaji wa maji safi na salama hivyo watafanyia kazi agizo la Mkuu wa Wilaya huku elimu ya utunzaji wa Maiundombinu ya maji ikiendelea kutolewa kwa wananachi.

Aidha Wadau na watumiaji wa maji wakichangia hoja zao katika kikao hicho walidai kuwa changamoto kubwa ni uharibifu wa miundombinu ya maji hususani kukata mabomba kwa kutumia mapanga na wakati mwingine kutupa mizoga ya wanyama kwenye matenki.

Licha ya agizo hilo Mkuu wa wilaya aliongeza kuwa kuanzia sasa sehemu yenye mradi itakayohujumiwa ikiwemo kungoa koki, kutupwa mizoga watendaji wa kata, wenyeviti wa vijiji na watendaji wa vijiji watachukuliwa hatua kali huku wananchi wakilipa vifaa hivyo.

“Nasisitiza tena kila mtu awe mlinzi wa miundombinu kifaa kimoja kikihibiwa lazima kijiji kizima mtaje mwizi au mtashiriki wote kununu kifaa hicho” aliongeza kusema Mkuu wa Wilaya.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post