NDEGE 80 KUTOKA URUSI ZATUA UTURUKI.


Ndege 80 kutoka Urusi zimewasili  nchini  Uturuki tangia kuondolewa kwa agizo la kufunga mipaka kutokana na covid-19.


Ndege 80 kutoka nchini Urusi zikiwa na watalii zimewasili nchini Uturuki ndani ya siku  baada ya kuondolewa kwa agizo la  kufunga mipaka lililotangazwa na serikali kama moa ya hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.


Watalii wengi kutoka nchini Urusi wameingia mkoani Antalya, mkoa  mmoja miongoni mwa mikoa ya  Uturuki ambayo huwa na idadi kubwa ya watalii katika msimu wa likizo ya kiangazi.


Eneo la Kusini  mwa Uturuki katika fukwe za bahari ya Mediterania  huwavutia watalii kwa mandhari yake ya kijani kibichi.


Kulingana na takwimu zilizotolewa na   uongozi wa  mikoa kuhusu utamaduni na utalii  Antalya, ni watu   zaidi  ya  milioni 5, 5 wametemebelea mkoa huo ni watalii kutoka nchini Urusi.


Safari za ndege  kati ya Uturuki na Urusi zilisitishwa  Machi  kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.


Watu  23,000 kutoka Urusi wameingia Uturuki  baada ya safari hizo kuanza upya.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post