MTANGAZAJI WA WASAFI AZIKWA ZANZIBAR.

 


Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha kijamii cha KWETU kinachorushwa na kituo cha televisheni cha WASAFI, Fatuma Abdalla 'Kungwi Mkatashombo' amezikwa siku ya jana Jumapili katika makaburi ya Mwanakerekwe, Zanzibar.


Shughuli za ibada pamoja na kuuga mwili zilifanyika nyumbani kwao Kinuni. Fatuma alifikwa na umauti siku ya Jumamosi mchana, na taarifa za kifo chake zilitangazwa na kituo chake alichokuwa anafanya kazi Wasafi TV.


Enzi za uhai wake Fatuma aliwahi kufanya kazi katika kituo cha radio Hits FM Zanzibar (kipindi cha Msisimko wa Pwani) baadae alihamia Wasafi Media na kufanya kipindi cha KWETU chenye vipengele vya KUNGWI na NGENDEBWE.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post