KIKOSI CHA JKT OLJORO CHATEKELEZA AGIZO LA RAIS LA KUJITEGEMEA KWA CHAKULA

Na Queen Lema Arusha

kikosi cha 833  kj Oljoro jkt kimenzisha mradi wa ngombe 70 na mbuzi 200 lengo likiwa ni kujipanga kuwalisha vijana  ambao wanajiunga na jeshi la kujenga taifa.

Hayo yamesemwa na kamanda wa kikosi hicho  Luten kanali   Joeli Meidimi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya themi njiro jijini Arusha kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea kufanywa na jeshi hilo kwa kuhakikisha kimejipanga kuwa na chakula cha kutosha.

Kanali medimi amesema kuwa wameanzisha mradi huo kufuatia maagizo yaliyotolewa na mkuu wa jeshi la kujenga taifa kwa makanda wote ya kuhakikisha wanakuwa na miradi ya vyakula vya kuwalisha vijana.

Ameongeza kuwa mbali na kikosi hicho  kujithatiti katiks uanzishwaji wa mradi huo lakini wamejipanga kulima mboga mboga ambapo kwa sasa wameanza kulima hekari 20 za mboga mboga kama shamba darasa pamoja na matumizi ya chakula.

Aidha amedai kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa kikosi hicho kinakuwa na chakula cha kutosha na miradi ambayo itawawezesha kukidhi mahitaji ya chakula kwa vijana wanaojiunga na jkt .

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post