DKT. CHARLES KIMEI AITEKA VUNJO , MOSHI

Na  Mwandishi  Wetu

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles  Kimei ambaye sasa ni mteule wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ubunge wa  jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro, leo amevunja rekodi kwa umati mkubwa uliojitokeza kumsindikiza  kurudisha fomu katika ofisi za tume ya uchaguzi mjini Moshi.Msafara mrefu uliojumuisha magari, Daladala, Bodaboda na Baiskeli ulimuongoza mgombea huyo aliyekuwa kwenye gari  la wazi kutoka nyumbani  kwake kijini Mamba, Marangu  mpaka kwenye ofisi za tume hiyo katikati ya mji wa Moshi.

 

Mmoja wasindikizaji aliyejitambulisha kwa jina la Enos Makundi alisema kuwa ni mara ya kwanza kwa historia ya jimbo la Vunjo, ambalo kwa muda mrefu limekuwa chini ya upinzani kumpokea mwana CCM kwa kishindo  kikubwa hivyo. “Kimei ameleta sura mpya katika siasa za Vunjo. Mara nyingi mapokezi haya walipewa wapinzani. Lakini ujio wa Kimei ambaye ni mzawa wa hapa mweye kukubalika na wengi, umeleta hamasa.Tunamuaminia” alisema.


 


Akizungumza baada ya kukabidhi fomu kwa Tume ya Uchaguzi mjini Moshi, Dokta Kimei ambaye ni mchumi mbobevu, alisema kuwa imani kubwa iliyopo kwa Raisi Magufuli, Chama cha Mapinduzi pamoja na yeye kama mgombea vimewapa matumaini mapya wana vunjo. “Nakishukuru sana Chama changu cha Mapinduzi CCM, chini ya Mwenyekiti Dokta John Pombe Magufuli, kwa kuniamini, na kunipa nafasi ya kugombea kuwawakilisha wana Vunjo. Hii ni heshima kubwa sana kwangu. Nawasihi wana Vunjo wote tuungane kwa maslahi mapana ya jimbo letu la Vunjo ili tulete maendeleo kwa kizazi kilichopo na kijacho.Leo napenda kuanza na shukrani kwa kila mtu aliyewezesha kuanza safari hii. Siku chache zijazo nitaeleza kwa undani mpango mkakati wangu, ambao naamini kwa kushirikiana na kila mwenye kuitakia mema Vunjo, tutafanikiwa.Pamoja Tunaweza ” alisema msomi huyo aliyezaliwa na kukulia katika Kijiji ca Komakundi, Kata Mamba, Marangu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post