WASIRA ATAMBA BADO ANA UWEZO KUSHINDA UBUNGE

MKONGWE  wa  siasa nchini Tanzania mbunge aliyekuwa ameondolewa madarakani na CHADEMA Steven Wasira  ametangaza nia ya kuutaka tena Ubunge wa Bunda Mkoani Mara kwa ticket ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo baada ya kutangaza nia baadhi ya Watu wameanza kumkosoa kwamba ana umri mkubwa hivyo anatakiwa kupumzika.

Wasira ambaye ana umri wa miaka 75 sasa hivi amesema “uwezo wa kuendelea kuwahudumia Wananchi wa Bunda kama wakinipa ridhaa upo ndio maana nimeamua kurudi na kuchukua fomu ya kuomba ridhaa”

“Kitu ambacho wengi wanakosea, Bunge ni kioo cha Jamii na ndio kinachowakilisha Watu wa Tanzania na Watu wa Tanzania wana marika yao, kuna Vijana, Wanawake, Wazee, Walemavu n.k kwahiyo Katiba haikusema ukifika umri flani huwezi kugombea”

“Na kwenye kugombea sipo peke yangu… wako Wazee wengi wanagombea mi sijui kwanini naulizwa mimi tu hahahahha…. Mzee Andrew Chege tunalingana umri na yeye anagombea kwanini wana-react upande wangu tu?”

“Hata hivyo kukosolewa hakunitoi mimi kwenye mstari, mimi nasoma maoni yote yanayoniunga mkono na yasiyoniunga mkono, wawaache wapiga kura wa Bunda waamue, kwanza stage tuliyonayo ni ya ndani ya Chama, tungoje kwanza Wanachama wa CCM kupitia Mkutano Mkuu wa Jimbo watatoa maoni yao”

“Kama wanafikiri hawahitaji Kiongozi mwenye umri wangu si wataninyima kura bwana……. lakini ukiona wamenipigia basi maana yake wanahitaji busara zangu na ushawishi wangu kwa ajili ya maendeleo yao, kwahiyo mimi sioni hoja ya reaction… sasa sijui reaction inatoka CCM au Upinzani… sielewi”

Chanzo ;millardayo.comThis is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post