WANAHABARI WAKONGWE WAMLILIA MKAPA

Mwanahabari George Semboni

WAKATI Taifa likiendelea kumlilia aliyekuwa  Rais wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa waandishi wa habari wawili wakongwe mkoni Tanga Paskal Mbunga na George Semboni
 Waeleza   namna walivyoishi nae katika sehemu mbalimbali za kazi. Mwandishi wa matukiodaima Amina Saidi anaripoti kutoka Tanga 

Waandishi hao wamemwelezea hayati Benjamin mkapa namna walivyomfahamu wakati wakiwa nae enzi za idara ya  habari(MAELEZO)na shirika la habari Tanzania( SHIHATA)kwamba alikuwa na msimamo thabiti jambo ambalo aliwataka walio kuwa chini yake waige mfano wake.

Mbunga alisema kwamba wakati alipokuwa anaandikia gazeti la Daily news akiwa katika kituo Cha Morogoro enzi za miaka ya 1976  hakuwahi kufanya nae kazi marehemu lakini  upepo uliendela kutawala katika ofisi hizo za gazeti la Serikali .

Aliongeza kwamba karibu waandishi wengi waliendelea kufuata utaratibu wanapokuwa ofisini navyumba vya habar wanakuwa makini na kazi bila kupiga makelele na vurugu wawapo ofisini.
Mwanahabari Paskal Mbunga

Alisema kuwa Beni Kama alivuokuwa anafahamika enzi hizo   alikuwa anatilia mkazo sana ubora wa uwandishi ulio wa umakini na wenye kufata maadili.

" Waandishi Kama Tommy Sithole) Mzimbabwe Frenk Mzirayi,Wenci Mushi walikuwa ni baadhi ya waandishi walionekana kufuata nyayo zake na hivyo baadae kufanikiwa katika taaluma ya habari " alifafanua Mbunga.


Kwa mfano alisema Frenk Mzirayi alikuja kuwa meneja mawasiliano wa mamlaka ya bandari( TPA) Dunfold Mpumilwa ambaye alikuja kuwa meneja wa kituo Cha kimataifa Cha mkutano( ACC)Tommy Sithole ambaye alikuja kuwa  mwariri mtendaji wa gazeti Herald la Zimbambwe baada ya nchi hiyo kupata uhuru.

Hata hivyo mzee Mbunga anakumbuka namna hayati Mkapa alivyoweza kujenga hoja aidha kwenye vyumba vya habar au katika mikutano na hoja hizo kukubalika kwa kauli moja.

Kwa upande wake Mzee George Semboni Alisema Marehemu alikuwa mkali kwa wale waandishi waliokuwa hawako makini na kazi.

" Kuna wakati mkapa anakuwa anasimama nyuma ya mwandishi anaeandika  habari anaisoma  na Kama hakuridhika nayo anaichomoa na kuichana mbele yake mwandishi na kumtaka mwandishi airudie tena aiandike kwa umakini zaidi" alisema Semboni.

 Hata hivyo Semboni anakumbuka namna Mzee Mkapa alivyokuwa anahimiza waandishi wa habari kuwa na upeo  mkubwa wa kuelewa  kazi yao ya uandishi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post