UTT AMIS YAZINDUA KITUO ARUSHA NA KUWATAKA WAKAZI WA MKOA HUO KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJ

Mwakilishi wa benki ya CRDB Mery Mponda akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji
wa maendeleo ya biashara UTT Amis Issa Wahichinenda wakilata utepe kuzindua kituo cha uwekezaji ndani ya jiji la Arusha mapema leo jijini Arusha
Mkurugenzi wa Uendeshaji
wa maendeleo ya biashara UTT Amis Issa Wahichinenda akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kituo chao mapema leo jijini Arusha


Mkurugenzi wa masoko UTT AMIS Daud Mbaga akiongea na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa kituo cha Utt Amis kwenye Jengo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro jijini Arusha mapema leo 

Mwakilishi wa benki ya CRDB Mery Mponda akiongea kwenye uzinduzi wa kituo cha uwekezaji tawi la Arusha kwenye jengo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro mapema leo jijini Arusha
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Utt Amis imezindua rasmi kituo cha kuhudumia wawekezaji katika
kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano kufikia uchumi wa kati wa
viwanda ambapo imetawaka wananchi mkoani hapa kuchangamkia fursa za
uwekezaji.

Akizungumza wakati akifungua kituo hicho katika jengo la mamlaka ya
hifadhi ya Ngorongoro lililopo jijini Arusha Mkurugenzi wa Uendeshaji
wa maendeleo ya biashara UTT Amis Issa Wahichinenda amesema kuwa
msingi huo umepelekea mfuko huo kusogeza huduma karibu kwa wateja.

Alisema kuwa mfuko huo wa utt Amis ni kampuni ya serikali yenye lengo
la uendeshaji wa mifuko 6 ya uwekezaji wa pamoja na kuwa wanatoa
huduma za usimamizi wa mitaji binafsi yote ikitekelezwa kwa sheria ya
masoko na mitaji ya dhamana ya mwaka 1994 na marekebisho yake na
kanuni za mifuko ya uwekezaji wa pamoja ya mwaka 1997.

Alieleza kuwa kuweka katika mifuko ya uwekezaji  wawekezaji
wananufaika na unafuu wa gharama za uwekezaji utaalam wa uendeshaji
kupitia meneja wa mfuko pia wawekezaji wanauwezo wa kufuatilia
uwekezaji wao na kujua hali ua uwekezaji wao na soko kwa ujumla.

Alisema kuwa mifuko hiyo imeandaliwa mahsusi kwa wawekezaji wadogo
kama vile mamalishe madereva bodaboda wachuuzi wadogo na wakubwa huku
ukuzingatia malengo yao ya uwekezaji muda wa kuwekeza ukwasi uwezo wa
kuhimili changamoto za uwekezaji na usalama.

“Mathalan mfuko wa umoja kiwango cha kuanzia kuwekeza ni vipande 10 tu
sawa na wastani wa takribani tsh.6500 huku mfuko wa uwekezaji maisha
unatoa faida pacha za uwekezaji ikiendana na bima ya maisha ya kiwango
cha chini tsh.8340 iwapo mwekezaji atachagua mpango wa kuwekeza kila
mwezi.

Awali mkurugenzi wa masoko wa UTT AMIS Daud Mbaga alisema kuwa msingi
wa mkuu wa wakazi wa mkoa wa Arusha ni kuchukuwa fursa hiyo kuwekeza
nao kwa kuendana na dhana ya serikali kufikia uchumi wa kati wa
viwanda.

Alisema kuwa kuanzishwa kwa mfuko huo wa uwekezaji wa pamoja yalikuwa
ni maksudi ya serikali kwa mwananchi wa chini kabisa kuwekeza fedha
zake kwa senti ndogo na kuendelea kukuza kipato chake kwa kuwekeza.

Nae Meneja wa CRDB alisema kuwa ushirikiano wao na mfuko huo wa
uwekezaji utasaidia kuongeza  tija za kiuchumi kwa wananchi wa hali ya
chini ambao wanahitaji kukuza mitaji yao kufikia malengo yao ya
kiuchumi.

Alisema kuwa wamekuwa wakishirikiana na mfuko huo bega kwa bega katika
zaidi ya matawi yao 10 yaliopo katika jiji la Arusha na mawakala wao
hivyo ufunguzi wa ofisi hizo utasaidia kuongeza tija kwa wananchi na
kusogeza huduma kwa umoja wao.

“Niwaombe wakazi wa mkoa wa Arusha kuitikia suala zima la uwekezaji wa
mfuko wa utt amis kwa lengo la kuisaidia serikali katika kuwaletea
maendeleo wananchi wake hivyo fursa hiyo sio ya kuicha iwapite hivi
hivi”alisema

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post