Rais Mstaafu Mkapa alivyoagwa leo Jijini Dar es Salaam

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William Mkapa wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa marehemu kitaifa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Julai 28, 2020 kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Mtwara kwa mazishi yatakayofanyika Julai 29, 2020.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 24, 2020.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William Mkapa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifuta machozi wakati akielezea namna alivyomfahamu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu, Benjamin William Mkapa.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya kitaifa ya kuuaga mwili wa marehemu Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.
Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani).
Mama Anna Mkapa ambaye ni mjane wa Hayati Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa akitoa heshima zake.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla hiyo ya kuuga mwili wa Mzee William Mkapa jijini Dar es salaam.
Msafara wa gari maalum ya JWTZ ikiwa imeubeba Mwili wa Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamin William Mkapa.
Mama Anna Mkapa ambaye ni mke Hayati Rais Mstaaf wa Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William Mkapa (aliyejifunika kitambaa cheusi) akiwa na wanafamilia baada ya kuwasili katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na viongozi wengine ambao ni Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia), Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kushoto) na Rais Mstaafu Mzee Alli Hassan Mwinyi (wa kwanza kushoto).
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia), Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan (wa tatu kushoto), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) wakiwa kwenye ibada ya kitaifa ya kuaga mwili wa Hayati Mzee William Mkapa jijini Dar es salaam.
Wageni waalikwa, wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na JWTZ wakitoa heshima kwa mwili wa Hayati Mzee William Mkapa jijini Dar es salaam. 
Baadhi ya Mawaziri wa SMZ na SMT pamoja na wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla ya kuuga mwili wa Hayati Mzee William Mkapa jijini Dar.
Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia), Waziri Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume Bunyoni (wa pili kulia), Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula (wa tatu kulia) pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa (wa pili kushoto).
Baadhi ya viongozi wa Serikali na Mawaziri wakifuatilia shughuli ya kuuaga mwili wa Hayati Mzee William Mkapa jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Rais Mstaaf wa Tanzania Hayati Benjamin Mkapa akizungumza kwenye shughuli hiyo.
Waziri Mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume Bunyoni akitoa salamu zake kwenye shughuli hiyo.
Kiongozi wa Mabalozi hapa nchini ambaye ni Balozi wa Comoro akitoa salamu wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Tanzania, Benjamin William Mkapa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Picha na Michuzi Blog

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post