MWANAFUNZI WA UDAKTARI APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUBAKA MWANAE WA KIDATO CHA TATU

Na Mwandishi Wetu, Njombe

Mwanafunzi wa Chuo cha udaktari  wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Mkazi wa Mburahati Jijini Dar es salaam na Itunduma kata ya Mtwango wilaya na Mkoa wa Njombe amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake na kumsababishia ujauzito.   
   
Akimsomea Mashitaka matano yanayomkabili mshitakiwa huyo Mwendesha Mashitaka wa Serikali Bi.Matrida Manja amesema mshitakiwa Joshua Mhema (26) alitenda makosa hayo katika nyakati tofauti huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Mwendesha mashtaka huyo aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa  alitenda makosa hayo Mei 06 na baadae aliendelea mfululizo Mei 26 na 27, 2020. Alisema kuwa katika zoezi hilo la kubaka Mei 27 alimpatia ujauzito mtoto wake huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ambayo jina lake linahifadhiwa kwa sasa.     
                      
Mshitakiwa alikana Mashitaka yote matano ambapo Mwanasheria wa Serikali Bi.Manja amesema mashitaka yote yanaangukia katika sura ya 130 (1&2) e kanuni ya adhabu na mwenendo wa makosa namba 16 yaliyofanyiwa marejeo mwaka 2016.      

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka makosa yote hayo matano yanadhamana na mtuhumiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika na kufahamika watakaosaini bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Tsh Milioni 15..       

Hata hivyo mtuhumiwa huyo alirejeshwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini hao na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 05 mwaka huu 2020 ambapo itaanza kusikilizwa kwa kuanza kutolewa ushahidi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post