MKUU WA WILAYA MONDULI ASISITIZA USHIRIKIANO

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Edward Balele amekutana na Viongozi, Watendaji na Wajumbe wa Serikali za Vijiji vya Emairete, Arkaria na Lendikinya. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kusisitiza Umoja na Mshikamano ili kuondoa changamoto  zilizoko kwenye jamii, ikiwemo migogoro ya ardhi.

Akizungumza kwenye majumuisho ya kikao hicho, Katibu Tawala wa Wilaya ya Monduli Komredi Robert Siyantemi, aliwataka wajumbe kuzingatia maadili ya uongozi ikiwemo dhana ya uwajibikaji wa pamoja.

"Watendaji wenzangu msipende kukimbilia Mahakamani. Tatueni migogoro yenu kwa njia ya usuluhishi kupitia Vikao vya Serikali za Vijiji na Vikao vya Kamati za Maadili za Chama cha Mapinduzi" alisisitiza Komredi Siyantemi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post