KURA ZA MAONI NJOMBE : Emmanuel Masonga Ashinda Kura za Maoni Jimbo la Njombe Huku Siglada Mligo Akishinda Ubunge Viti Maalumu kwa asilimia 82.3.

waliokuwa wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombe wa nafasi za ubunge wakiwa katika mdahalo

Na Mwandishi Wetu, Njombe


Chama cha demokrasia na maendeleo chadema jimbo la Njombe kimefanya uchaguzi wa kura za maoni na kufanikiwa kuwapata wagombea wawili ambao licha ya kushinda katika kura za maoni kwa kishindo lakini majina yao na wale ambao kura hazikutosha yatafikishwa katika meza ya kamati kuu ili kuchakatwa zaidi na kisha kutoa uamuzi wa mwisho wa atakaepewa ridhaa na chama kuwania Ubunge.

Akitangaza matokeo ya watia nia wa kiti cha ubunge viti maalumu jimbo la Njombe mjini msimamizi wa uchaguzi huo Leonce Marto amesema wapiga kura walikuwa 34 na mtia nia Mairieth Joseph Mwalongo amepata kura 0,Enioth Elias Laizer kura 1, Lucia Mlowe kura 2,Rose Mayemba kura 3 na Siglada Mligo amepata kura 28 sawa na asilimia 82.3 na kuibuka kidedea katika uchaguzi huo

Msimamizi katika uchaguzi huo Lazaro Nyaladu akiwa katika picha ya pamoja na washindi
Katika uchaguzi wa kura za maoni kwa kiti cha ubunge wa jimbo hilo Marto amesema Wagombea walikuwa wanne na mgombea Marieth Mwalongo amepata kura 0 , Lucia Mlowe amepata kura 11, Rose John Mayemba amepata kura 26 ambayo ni sawa na asilimia 22.6 huku Emmanuel Masonga akiibuka kidedea kwa kupata kura 78 ambayo ni sawa na asimilia 67.8.

Kukamilika kwa uchaguzi huo kunafungua milango kwa kamati kuu ya chama kufanya maandalizi ya utezi wa mwisho kwa wagombea ubunge kwa majimbo yote 264 zoezi ambalo litafanyika baada ya  mkutano mkuu kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Mara baada ya kutangaza matokeo ya watia nia wote ndipo msimamizi wa uchaguzi bwana Leonce Marto akatoa nafasi kwa wagombea ambao kura hazikutosha na wale walioibuka kidedea ambao kwa kauli moja wakakubaliana kuvunja kambi na aina yoyote ya makandi ili kuichia kamati kuu kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu nani anastahili kupeperusha bendera ya chama baada ya kupitia na kuchakata taarifa za watia nia wote.

Kabla ya kufanyika kwa zoezi la kura za maoni jimbo hilo lilifanya mdahalo uliokutanisha watia nia wote wa ubunge ili kupima uwezo wao wa kujenga hoja na kutetea kwa lengo la kumpata mgombea ambaye hata acha shaka kuhusu uwezo wake katika utetezi wa haki za wapiga kura wao.This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post