ASAS YA HVO YATOA MSAADA WA ZAIDI YA TSH MILIONI 12


  ASASI isiyo ya Kiserikali ya Hope Village Organization (HVO)imetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya sh, Milioni 12 kwenye kituo cha Afya cha Halmashuri ya Madaba Wilaya ya songea mkoani Ruvuma ili viweze kuwasaidia wauguzi na wagonjwa katika kituo hicho.Mwandishi Amon Mtega anaripoti kutoka Ruvuma 

 Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo  mkurugenzi wa Asasi hiyo Nashon Kikalao amesema kuwa asasi hiyo imeamua kutoa msaada wa vifaa hivyo ili kuunga mkono jitihada za serikali katika utekelezaji wa huduma mbalimbali za jamii ikiwemo Sekta ya Afya.

  Kikalao amesema kuwa Serikali imekuwa ikijitahidi katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Afya hivyo ni vema jamii na mashirika mbalimbali yakatambua jitihada hizo kwa uunga mkono katika uwajibikaji wakujitolea .

  Mkurugenzi huyo alianisha baadhi ya vifaa walivyokabidhi kwenye kituo hicho kuwa ni pamoja na mitungi ya hewa (Oxygen cylinder)ambayo itawasidia wagonjwa pindi wanapotakiwa kupatiwa msaada wa mashine ya kupumulia na kuwa  vifaa vyote vimenunuliwa hapahapa Nchini kwa kushirikiana na ofisi ya Afya ya Madaba.

    Kwa upande wake mganga mkuu wa Halmashauri ya Madaba Dr.Mussa Rashid wakati akivipokea vifaa hivyo alisema kuwa ni vifaa bora ambavyo vitasaidia katika kituo hicho cha Afya.

 Rashid akivipokea vifaa hivyo kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Shafii Mpenda amesema kuwa awali kulikuwa na upungufu wa baadhi ya vifaa hivyo lakini kutokana na msaada huo utaenda kupunguza tatizo hilo .

  Aidha amesema kuwa Serikali imefanya mambo mengi ikiwemo katika Sekta ya Afya kwa kuboresha miundombinu yake ikiwemo kuyajenga majengo mazuri yenye viwango pamoja na huduma za dawa kupelekwa kwa wakati.

  Ikumbukwe kuwa kituo hicho cha Madaba ndicho kituo pekee ambacho majengo yake mapya yalijengwa na serikali ya awamu ya tano yalipatiwa bahati ya kuzinduliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli pindi alipofanya ziara mkoani Ruvuma mwaka 2019 kwa niaba ya vituo vingine vya hapa Nchini .

                                            MWISHO.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post