DIWANI AGAWA BARAKOA, VITAKASA MIKONO

Diwani wa kata ya Bomambuzi na Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi  Manispaa Ya Moshi Juma Raibu akiwafundisha wananchi namna ya kuvaa barakoa(picha na Woinde Shizza, Kilimanjaro)
Na Woinde Shizza , KILIMANJARO

Diwani wa kata ya Bomambuzi na Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi  Manispaa Ya Moshi Juma Raibu amekabidhi Barakoa 100, vitakasa Mikono,  pamoja na Ndoo Kwa wafanyabiashara wa Soko la pasua Mjini Moshi ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona  ambavyo vinaendelea kutikisa dunia.

Akiongea wakati  akikabidhi vifaa hivyo Diwani huyo alibainisha kuwa ameamua kutoa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa wananchi hao ,ili waweze kuokoa maisha yao na kuwa na tahadhari ya ugonjwa huo wakati wote.

Amesema kuwa mbali na kutoa vifaa hivyo pia ameweza kugawa elimu ya kujikinga na ugonjwa hatari wa Corona kwa wananchi wa kata ya Bomambuzi pamoja na wafanyabiashara wa masoko ya pasua na  mbuyuni huku akibainisha kuwa wataendelea kutoa vifaa vya kujikinga na elimu kwa kila mwananchi.

Aidha aliwaasa Wananchi hao kufuata Maelekezo ya Wataalamu wa Afya na Maagizo Ya Serikali huku wakizingatia zaidi  Kuepuka Misongamano Isiyo Ya Lazima. 

Pia Diwani huyo aliwaonya wananchi wanaopotosha jamii kuhusu  idadi ya wagonjwa pamoja na  wanaofariki kwa virusi vya Corona na kusema kuwa  iwapo atabainika mtu anafanya hivyo hatua Kali zitachukuliwa dhidi yake, huku akiliagiza jeshi polisi kuwachukulia hatua kali za kisheria.


Amesema wamehamasisha jamii juu ya kuweka na kunawa na maji tiririka na sabuni kwenye sehemu zote za biashara nyumbani na maeneo yote yenye mikusanyiko.

Akishukuru kwa msaada huo mmoja wa  wafanyabiashara wa soko la Pasua Gloria Mboya alisema kuwa anashukuru kwa diwani huyo kwa kuendelea kuwajali wananchi wake  kwa kuwapa vifaa vya kujikinga pamoja na kuwapa elimu ya namna ya kuendelea kuchukuwa tahathari ya ugonjwa huo.

Alisema kuwa ugonjwa huo upo hivyo ni vyema kila mtanzania  kuendelea kujikinga na kufuata maelezo yanayotolewa na wataalam,huku akikisitiza kuwa iwapo mtu yeyote akijihisi anadalili za ugonjwa huo kuwa maramoja hospital kwa ajili ya kupata  huduma.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post