WATUMISHI HOUSING COMPANY YASHAURIWA KUTENGA NYUMBA ZA KUWAUZIA NA KUPANGISHA WADAU WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

Baadhi ya Nyumba za ghorofa za Mradi wa Watumishi Housing Company zilizojengwa kwa madhumuni ya kuuziwa Watumishi wa Umma na kupangishwa katika eneo la  Gezaulole Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary akitoa ushauri juu ya upangishaji na uuzaji wa nyumba kwa watendaji wa Watumishi Housing Company katika mojawapo ya nyumba alizozikagua eneo la Gezaulole  - Kigamboni jijini Dar Es salaam.
Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa akitoa maelezo kuhusu mradi wa nyumba za kampuni hiyo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi ujenzi wa nyumba eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akikagua nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Company eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company Dkt. Fred Msemwa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post