TCRA CCC YAPOKEA CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM -PATANDI

 Anayezungumza ni Katibu Mtendaji kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma za mawasiliano Tanzania (TCRA CCC )Mary Shao Msuya,kulia kwake ni Mhandisi mwandamizi TCRA Jan Kaaya ,akifuatiwa na mjumbe wa Baraza
Mmoja wa wanafunzi mwenye ulemavu wa ngozi na uoni hafifu kutoka Chuo cha Ualimu Patandi akiuliza swali kwa Baraza la Usahauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Tanzania 
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha ualimu Patandi waliojikusanya kwaajili ya kupatiwa elimu juu ya matumizi sahihi ya huduma ya mawasiliano na mitandaoya kijamii kutoka TCRA CCC
 Kutoka kushoto ni Mhandisi Mwandamizi TCRA Jan Kaaya akifuatiwa na Katibu Matendaji kutoka TCRA CCC wakiwa Chuo cha Ualimu Patandi . Na.Vero Ignatus,Arusha

Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma Mawasiliano  Tanzania TCRA CCC limepokea maoni pamoja na changamoto za kutoka kwa  walimu na wanafunzi wenye mahitaji maalum katika chuo cha Ualimu cha Patandi kilichopo mkoani Arusha na kuahidi kuyatendea kazi

Akizungumza mara baada ya baraza hilo  kutembelea chuoni hapo na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mawasiliano na mitandao  ya kijamii Katibu mtendaji baraza hilo Mary Shao Msuya alisema kuwa ni zoezi  endelevu kwaajili ya kutoa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano nchini.

Amesema kuwa baadhi ya changamoto nyingine wamezijibu hapohapo ila nyingine wamezichukua na kuondoka nazo ili kuona namna gani wataweza kuboresha huduma hizo za mawasiliano ili kila mtu aweze kuzitumia kwa manufaa na makusudiao halali anayotaka kuyafanya

‘’Tumshauriana nao na tumepokea maoni kutoka kwao  pamoja na changamoto mbalimbali za huduma ya mawasiliano tumebadilishana mawazo walikuwa na maswali mengi mengine tumeyajibu,mengine tunaenda kuyatendea kazi alisema Shao’’
Shao aliwakumbusha watumiaji wa huduma hizo za mawasiliano kuanza kujilinda wao wenyewe kwanza  na kuwa makini na watumiaji wengine ambao siyo waaminifu ambao wanatumia uhalifu kama fursa kupitia mitandao hiyo kutokuwa wepesi wa kujibu jumbe wanaz otumiwa na watu ambao hawawafahamu

Kwa umoja wao  baadhi ya wanavyuo wenye ulemavu walioshiriki na kupata elimu hiyo wameipongeza TCRA CCC Kwa kuwatahamini na kuona umuhimu wao na kuwatembelea chuoni hapo wamewaomba wasichoke bali pale kutakapokuwa na madadiliko yeyote katika huduma ya mawasiliano wawatembelee na kuwaelimisha Zaidi.

Kwa upande wake Mtoa  Elimu kutoka TCRA CCC Hillary Tesha alisema kuwa mtumiaji wa bidhaa au huduma za mawasiliano anaweza kuwasilisha malalamiko kwa muuzaji au mtoa huduma ambapo mtoa huduma atatakiwa kushughulikia na kujibu kwa mlalamikaji hatua zilizochukuliwa ndani ya siku thelathini (30)

Alisema endapo kama mtumiaji hakuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na mtoa huduma au bidhaa mlalamikaji anaweza kupeleka malalamiko yake kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post