
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amesema mtuhumiwa Lema amekamatwa jana jioni mjini Arusha na kisha kusafirishwa hadi Singida mjini.
Amesema hivi karibuni Lema alipokwenda Manyoni kuhudhuria mazishi ya dereva wa boda boda Alex Joas alitumia fursa hiyo kupotosha wananchi kwamba Jeshi la Polisi halikuchukua hatua zozote dhidi ya matukio ya mauaji ya wakazi 14 Wilaya ya Manyoni.
Njewike amesema Lema atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.