UWAJIBIKAJI CHACHU KUIMARIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NA KUONDOA CHANGAMOTO NDOGO NDOGO ZA UKOSEFU WA FEDHA

Na Ahmed Mahmoud Arusha
 Image result for jumuiya afrika mashariki
Imeelezwa kuwa changamoto za ukosefu wa fedha ndani ya Sekretariet ya jumuiya ya Afrika Mashariki bado zipo ila sio kama ilivyokuwa awali.

Hayo yalielezwa na Mbunge wa Bunge la EALA Mariam Ussi Yahaya baada ya kutokea mjadala mkubwa wa suala la ukosefu wa fedha za kuendesha Jumuiya hiyo ndani ya bunge la EALA baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya ukaguzi wa fedha wiki iliyopita.

Alieleza kwa hapo awali kulikuwa na ubadhirifu mkubwa Ila baada ya bunge kuisimamia kidete ubadhirifu umepungua kwa kiasi kikubwa hivyo kuifanya suala hilo kuweza kubana matumizi yanayosaidia kuendelea kwa shughuli za kila siku kwa kuwa jumuiya bado ni ndogo hivyo changamoto ndogo ndogo lazima ziwepo.

Alisema kuwa ripoti hiyo ni nzuri tofauti na huko nyuma Ila inatakiwa kwenda na muda halisi ipo nyuma miaka miwili tunahitajika kwenda na muda uliopo kwa kuwa watu wapo kiuwajibikaji itasaidia kuondoa changamoto ambazo zimebakia sio kama jumuiya imeshindwa kuondoa ubadhirifu ni muda tu tutamaliza changamoto hii.

Kwa mujibu wa mbunge huyo kuimarika kwa jumuiya na shughuli zake kunatokana na Bunge hilo kuongeza usimamizi wake hivyo sio kwamba ubadhirifu utaendelea kukua bali ndio wameendelea kusaidia kuondoa tatizo hilo kuifanya jumuiya hiyo kuongeza ufanisi na kuimarika.

"Sioni sababu ya kuendelea au kuweka sheria kali za kusimamia kwa kuwa jumuiya hii inaendesha shughuli zake kwa maridhiano ya mkataba wake hivyo naona jumuiya ikiendelea kuimarika siku hadi siku na ubadhirifu au ukosefu wa fedha sio kikwazo wala changamoto kubwa kwa Sasa"

Kwa Upande wake Mbunge wa Bunge hilo George Odongo alisema kuwa mjadala wa ripoti ya ukaguzi wa Fedha utasaidia Sana kuongeza nidhamu na uwajibikaji miongoni mwetu kusaidia kuongeza ufanisi na jumuiya kuendelea kuimarika.

Alisema kuwa msingi mkubwa wa jumuiya kuendelea ni kusimama na suala zima la uwajibikaji na kutanguliza mapenzi makubwa ya mtangamano ambayo wananchi wetu ndio waliotufanya tuwe hapa kuendeleza udugu utakaosaidia kuendeleza Umoja wetu.

"Nakumbuka Sana waziri wetu wa Uganda alisema hapa nchini Tanzania mwalimu Nyerere aliwahi kusema watanzania wafunge mikanda ili kuweza kukomboa nchi zetu za bara la Afrika Umoja ndio msingi wa waafrika kuweza kufanikiwa kwenye jambo lolote nasi bunge tupo kuisimamia kuweza kuimarisha umoja huu"

Akiongelea suala la Muswada wa sheria ya madini ambayo bunge hilo limefikia mahali pazuri kwa kuangalia sheria za Tanzania kama njia ya utungwaji sheria za mataifa hayo ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kusema sheria inaweka wazi nchi yenye sheria nzuri zitumike na wanajumuiya.

Nae Mbunge wa Eala Mhandisi Suzan Masay alisema kuwa suala la ukosefu wa fedha ni pana linahitaji Baraza la mawaziri kulipatia ufumbuzi wa kudumu ili kuona wafanyakazi wakipata stahiki zao Tena kwa wakati na wafanyakazi waweze kuwajibika kuendelea kuimarisha misingi ya uwajibikaji.

Alieleza kuwa msingi mzuri wa wafanyakazi kupata.stahiki zao ndio jukumu la kuendesha Jumuiya kwa kuwa kila mmoja kwa nafasi yake awe mtafiti aweze kutekeleza ndani ya muda uliopangwa kusaidia shughuli za jumuiya kutokwama hivyo suala hili liangaliwe kwa umakini mkubwa Sana.

Suala la wafanyakazi ni suala gumu kidogo tumekuwa tukisubiri mabadiliko ya kisheria ambayo yakikamilika yatasaidia kuondoa changamoto hiyo na kuendelea kuimarisha misingi ya uwajibikaji ndani ya jumuiya yetu tusubiri wakikamilisha suala hilo itakaa sawa.

"Jumuiya yetu inaendesha shughuli zake kwa kutegemea michango kutoka kwa nchi wanachama na wafadhili Sasa fedha zikiwa kidogo kutokana na michango ya nchi hizo na wafadhili wakichelewesha fedha ndio changamoto inaanzia hapo suala hili linazungumzika na kila hatua tunayopiga kama jumuiya inahitaji maridhiano ya pamoja"

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post