MSIMAMO WETU NI KUSIMAMIA YALE TULIYOAHIDI KWA WANANCHI ASEMA ZELOTHE

 Image result for mwenyekiti wa ccm mkoa wa arusha zelothe
Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Zelothe Steven ameeleza msimamo wa Chama hicho kwa wananchi ni kusimamia utekelezaji wa ilani yake walioahidi kwa wananchi mwaka 2015 na sio vyengine.
Aliyasema hayo kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani  kwenye ziara ya kamati ya siasa ya CCM Mkoa na kutembelea miradi  mbalimbali ya maendeleo katika Jiji la Arusha katika ziara hiyo alisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Joseph Massawe, wajumbe wa CCM sekretarieti ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Arusha . Gabriel Daqarro pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni.
Alisema kuwa amerishishwa Sana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo imeelekezwa kumrahisishia mwananchi kupata huduma bora za kijamii ikiwemo maji elimu Afya na miundombinu ya usafirishaji sanjari na nishati ya umeme.
Zelothe Steven alipata nafasi ya  kutembelea mradi mkubwa wa maji uliopo  Ngaramtoni ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi wa kumi na mbili mwaka huu ikiwa dhumuni kubwa la mradi huo ni kuboresha hali ya upatikanaji wa maji  kwa maana ya kuongeza mtandao wa kuwasambazia wananchi maji safi.
Akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi wa AUWSA  Mhandisi Gasto Mkawe amesema mradi huo ni sehemu ndogo tu  ya mradi mzima kwani mradi wenyewe umegawanyika katika vipengele vitatu ili kurahisisha utekelezaji  wake  ambapo mradi wote kwa ujumla  utagharimu shilingi billion 520 za kitanzania pia amebainisha kuwa uzalishaji wa maji utaongezeka kwa wastani wa lita 40,000,000 hadi lita 200,000,000 kwa siku.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo alimpongeza Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapatia fedha hizo pia amefurahishwa na kasi ya mkandarasi aliyepewa jukumu la kukamilisha mradi huo kwa kasi ya utekelezaji anayofanya.
Mhe. Zolothe Steven pia alitembelea mradi wa barabara ya Ngaramtoni  inayoenda mpaka Usa River barabara ya (By pass) Jijini Arusha. Ujenzi wa barabara hiyo ya lami yenye urefu wa kilomita 42.4 kutoka Ngaramtoni hadi Usa River ambayo ikikamilika,  itapunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Arusha mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 139 fedha za Kitanzania.
Sambamba na hilo Zelothe alitembelea mradi  mwingine mkubwa wa maji Jijini Arusha Olasiti (Burka Tenki la maji) ambao ume gharimu shilingi bilioni 2.3 akiwasilisha taarifa ya mradi huo amedokeza kuwa mradi huo utapokea maji kiasi cha lita milioni 3 kutoka katika tenki linguine kubwa lililopo Ngaramtoni.
Naye Mhandisi Gasto Mkawe  alisema wanufaika wa mradi husika ni wakazi wa Kata za Olasiti, Sombetini, Osunyai, Sokoni 1, Murieti, na Terrati wapatao 156,320 nakuongeza kuwa pamoja na tenki hili kujengwa pia AUWSA imepanga kujenga matenki mengine 11 katika maeneo mengine likiwemo lile la Ngorbob, Olmoti, Mlima ccm,Themi, Moshono, Moivo na mengineyo.
Ziara hiyo iliendelea hadi kituo cha Afya Murieti  mbapo Mhe Zolothe alipokea taarifa ya utekelezaji  kutoka kwa Mganga Mkuu wa Jiji Dkt. Simon Chacha.
Dkt. Chacha alisema  kuwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho ume gharimu jumla ya  shilingi  bilioni moja  milioni miamoja sabini na tisa mianne arobaini kati ya fedha hizo fedha, milioni mianne sabini na tisa mianne arobaini zimetolewa na Halmashauri ya jiji la Arusha kwa maana ya makusanyanyo ya ndani na Serikali kuu ilitoa  jumla ya shilingi milioni miasaba . pia ameishukuru serekali ya Jamuhuri ya muungano chini ya Mhe. Dkt. Joh Pombe Magufuli kwakutoa  fedha zilizo saidia kukamilika kwa mradi huo.
DktChacha alidokeza kuwa kituo hicho kimeanza kutoa huduma za kumuona Daktari, maabara, kulaza wagonjwa kwa mda pia huduma za VVU na UKIMWI , huduma za mama na mtoto pamoja na upasuaji mdogo na kusema kuwa kabla ya mwezi huu  kuisha kituo hicho kitaanza kutoa huduma za upasuaji kwa kina mama
Dkt. Chacha alisema kuwa lengo kubwa ni kusaidia kata ya murieti yenye Wananchi wapatao 56,000 alieleza kuwa kata hiyo ina mitaa 13 lakini kata yote haikuwa na kituo cha afya. Baadaye Mhe. Zelothe alitembelea Shule ya Sekondari ya Arusha Terrat, mradi wa maji machafu uliopo Terrat ambao upo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake, Hospitali ya Wilaya ya Engutoto na kituo cha afya Moshono.
Mhe. Zelothe Steven amefurahishwa na utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo  alisema pia ilani inayo itekelezwa  ni  ilani ya CCM inayo elekeza kuwa kila Kata iwe na kituo cha afya na uboreshaji wa miundo mbinu kwa hali ya juu. “Kwa hiyo  Serikali ya CCM ni dhahiri kusema kwamba inatekeleza kile walicho ahidi kwa wananchi wake nakuwaahidi kwamba hayo ni matokeo ya awali yapo matokeo mazuri  yanafuata” alisema Zeloth.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post