KATIBU WA CCM JAMHURI MBARONI AKITUHUMIWA KWA UBAKAJI

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Katibu wa CCM Tawi la Jamhuri kata ya Daraja mbili jijini Arusha,Aron Sanare Kivuyo anashikiliwa na jeshi la Polisi Jijini hapa kwa kosa la kumbaka na kumpatia ujauzito mwanafunzi wa kituo cha Compassion Mwenye umri wa miaka 15 baada ya kumrubuni kwa fedha na mahitaji mbalimbali aliyokuwa akimpatia

Aroni Mwenye umri wa miaka 56 mkazi mtaa wa Sanare,Daraja mbili anadaiwa kumpachika ujauzito mwanafunzi huyo  baada ya kumrubuni kwa kumpatia fedha na mahitaji mengine mbalimbali na baadae alimwomba fadhila ya ngono jambo ambalo alifanikisha adhima yake.

Diwani wa kata ya daraja mbili Prosper Msofe amethibitisha kukamatwa na kushikiliwa kwa kiongozi huyo wa ccm katika kituo cha polisi jijini hapa na kueleza kuwa wao kama viongozi wanalaani vitendo vya ubakaji na kulitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa tukio hilo na sheria ichukue mkondo wake.

Akizungumzia sakata hilo mratibu w
a kituo cha Student Center (P.A.G )kilichopo Unga LTD jijini hapa, chenye ushirika na shirika la Compassion Tanzania,mratibu wa kituo hicho,Yona Kaaya amesema kuwa walifanikiwa kugundua ujauzito wa mwanafunzi huyo Mara baada ya kuona mabadiliko ya kiafya.

Amesema kuwa mwanafunzi huyo ambaye jina linahifadhiwa amekuwa akiishi na mlezi wake katika mtaa wa Sanare na kusoma masomo mbalimbali katika kituo hicho lakini juzi jumatatu alipelekwa kupimwa ujauzito katika hospital ya Mount Meru na kugundulika kuwa anaujauzito na kumtaja katibu huyo wa ccm kuwa ndiye mhusika Mkuu wa kupachika mimba watoto wadogo

Kwa upande wake baba mlezi wa msichana huyo Boniface Mbwambo amesema kuwa amekuwa akiishi na msichana huyo ambaye ni mtoto wa shemeji yake na kwamba tukio la kubakwa na kupewa ujauzito limemshitua sana.

"Nimegundua kuwa mtoto anaujauzito kutoka kwa wadhamini wake wanaomsomesha hapo Compassion Mimi kama mzazi wake mlezi nimesikitishwa sana ukizingatia aliyempa huo ujauzito ni kama babu yake " Amesema Mbwambo.

Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Gabriel Gadarro amekuwa akiionya jamii kuacha kuficha matukio hayo na kupatana kutumia mila na desturi na kueleza kuwa serikali ya wilaya kwa kushirikiana na vyombo vya dola imeandaa mkakati wa kuhakikisha matukio ya namna hiyo yanafiklchuliwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post