Kamati ya Amani Mkoa wa Mbeya yaahidi Kupeleka ujumbe kwa waumini.

Kamati ya Amani mkoa wa Mbeya wameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoa elimu juu ya utumiaji wa huduma za mawasiliano kwa kujinga na Uhalifu unapotumia hudima hizo.

TCRA iko katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja ambayo umeanza mkoani Mbeya ambayo itazunguka nchi nzima kutoa elimu hiyo.

Viogozi wa dini wa Kamati Amani Mkoa wa Mbeya wamesema Kampeni hiyo umefika wakati mwafaka kutokana na sekta ya Mawasiliano kukua kwa kasi .

 Viongozi hao wamesema  elimu waliopata TCRA wataipeleka kwa waumini wao katika e ya kujikinga  na uhalifu  wanapotumia huduma za mawasiliano.

Viongozi hao wamedai kuwa ni kupeleka elimu waumini ikiwa  mchango wao kwa ustawi  wa nchi yetu

Wameyasema hayo  walipokuwa  semina  ya kuelimisha jinsi ya kujikinga na uhalifu wakati wa kutumia huduma za mawasiliano  ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Sirubiniki Mjanja  haingizwi  chaka  inayolenga  katika kuelimisha umma ya kujikinga.

Mkuu wa Nyanda za Kusini Asajile John akizungumza na Kamati ya Amani Mkoa wa Mbeya kuhusiana na Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja ya Uhalifu katika Semina iliyofanyika jijini Hapa.
Akichangia mada Sheikh wa Wilaya Abdallah Omari amesema  semina hiyo ni kuwapongeza TCRA  katika  kuwalinda  wateja na kuahidi  kushiriki katika  kampeni  hiyo.

Mmoja wa Viongozi wa Dini Askofu wa Msaidizi wa Anglican Daud Sichinga  ametoa  wito  kwa taasisi  nyingine  kuiga mfano  wa TCRA katika  kuelimisha  umma kwani viongozi wa dini wanawafuasi wengi  na ushawishi  mkubwa  katika  jamii.


 Kampeni  ya Sirububiki  Mjanja haingizwi  chaka  imeandaliwa  na Mamlaka ya Mawasiliano  kushirikiana na Jeshi  la polisi  kitengo cha uhalifu  mitandaoni  yenye lengo la kuelimisha  jamii jinsi ya kujikinga  ili wasirubuniwe wanapotumia  huduma za mawasiliano.

Kampeni  ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka  inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania
 Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu  mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo  la kujenga  maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali

Nae Mkuu wa Kanda ya Nyanda za  Juu Kusini wa TCRA Asajile John amesema kuwa viongozi wa dini ni watu mhimu sana katika kutoa elimu kwa waumini.

Amesema kuwa huduma za mawasiliano ni pana sana na teknolojia yake inabadilika kila siku 

John amesema TCRA itaendelea kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya Mawasiliano kuhakikisha yanakuwa salama  kwa ustawi wa nchi.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.
Amesema wakati amefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi  pamoja na wanatumia mawasiliano vibaya mkono wa sheria utawakuta.
Baadhi wa wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Mbeya wakiwa katika Semina ya TCRA ya Kujikinga na Uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano ikiwa ni Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.
Askofu Msaidizi, Kanisa la Anglican Mbeya Daud Sichinga akichangia mada katika Semina ya Kamati ya Amani Mkoa wa Mbeya

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post