WAASI WA YEMEN WANAOUNGWA MKONO NA IRAN WAUA WANAJESHI 80


Zaidi ya wanajeshi 80 wa Yemen wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la kombora na ndege zisizokuwa na rubani linalodaiwa kufanywa na waasi wa Houthi. 


Shambulizi hilo linafanywa baada ya miezi kadhaa ya utulivu katikati ya vita kati Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran na serikali ya Yemen inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa inayoungwa mkono na majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia. 

Vyanzo kutoka hospitali ya Marib ambako wahanga wa shambulizi hilo walipelekwa, vinasema wanajeshi 83 waliuawa na 148 walijeruhiwa. 

Shambulizi hilo linakuja siku moja baada ya muungano unaosaidiwa na majeshi ya serikali kuanzisha operesheni kubwa dhidi ya Wahouthi katika eneo la Nihm, kaskazini mwa mji mkuu Sanaa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post